ASKOFU Mkuu wa Makanisa ya Karmeli Assemblies of God Tanzania (KAG), Dkt. Evance Chande, amewataka wanasiasa kuacha chuki bali kinachotakiwa ni kujifunza kupitia Dabi ya watani wa jadi Yanga na Simba ambayo daima wakishindana huishia kutaniana badala ya kupigana au kuzua magomvi. Aidha amewataka watanzania kukataa migawanyiko na kuwa makini dhidi ya watu wanaochochea mifarakano, akisisitiza kuwa kukubali hali hiyo kunaweza kuhatarisha umoja, amani na utulivu wa nchi. Akizungumza Novemba 8, 2026, katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Kanisa la KAG, eneo la Lugala, Nala jijini Dodoma, Askofu Chande alisema wananchi wana wajibu wa kulinda umoja wa taifa kwa kutoruhusu tofauti mbalimbali kutumiwa kuwagawanya. Alisisitiza kuwa kila mmoja anapaswa kuwa sehemu ya kuimarisha mshikamano badala ya kuunga mkono vitendo vinavyoweza kuleta mifarakano katika jamii. Kupitia harambee hiyo, jumla ya Sh milioni sita zilichangwa papo kwa papo, huku washiriki wengine wakitoa ahadi za kuchangia fedha kwa ajili ya kufanikisha hatua hiyo ya ujenzi. Ujenzi wa kanisa hilo kubwa umefikia hatua ya linta, hatua inayotangulia kuendelea na kazi nyingine za ujenzi kuelekea kukamilika kwa jengo hilo. Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini kutoka madhehebu tofauti, waliotoka ndani ya Dodoma na mikoa mingine, ikiwa ni sehemu ya kushiriki tukio hilo la uwekaji wa jiwe la msingi.
𝗠𝗮𝗸𝗮𝗯𝗶𝗹𝗮 10 𝗮𝗺𝗯𝗮𝘆𝗼 𝘂𝗸𝗶𝗸𝗮𝗮 𝗸𝗮𝗿𝗶𝗯𝘂 𝗻𝗮𝗼, 𝗸𝘂𝘁𝗼𝗯𝗼𝗮 𝗸𝘂𝗻𝗮𝘄𝗲𝘇𝗮 𝗸𝘂𝘄𝗮 𝗿𝗮𝗵𝗶𝘀𝗶 𝘇𝗮𝗶𝗱𝗶 ⚠️ Kumbuka: Haya ni maoni na mitazamo ya kijamii tu, si kwamba kabila fulani lina mafanikio kuliko lingine. Mafanikio yanategemea juhudi, elimu, nidhamu na fursa. 1. Wasukuma Wana sifa ya kufanya kazi kwa bidii, hasa kwenye kilimo, ufugaji na biashara. Wengi huaminika kuwa wavumilivu katika kutafuta maendeleo. 2. Wachagga Hujulikana kwa moyo wa biashara, uwekezaji na kusaidiana kifamilia katika shughuli za maendeleo. 3. Wahaya Wana historia ndefu ya biashara, elimu na shughuli za uzalishaji zinazochochea maendeleo. 4. Wanyakyusa Wengi wanasifiwa kwa bidii katika biashara, kilimo na uwekezaji wa muda mrefu. 5. Wakinga Hujulikana kwa uchapakazi, nidhamu na uthubutu wa kutafuta fursa sehemu mbalimbali za nchi. 6. Waha Wana sifa ya kujituma katika biashara na shughuli mbalimbali za kiuchumi. 7. Wapare Mara nyingi husifiwa kwa kuthamini elimu, kazi na mipango y...

Comments