CHELSEA YAIBAMIZA BOLTON 4-0

Timu ya Chelsea file pix

BOLTON, England
DIDIER Drogba alifunga bao la aina yake katika
mechi ya Ligi Kuu ya England ambayo Chelsea
iliibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Bolton
kwenye uwanja wa Reebok.
Drogba alipiga shuti kali la mita 33 ambalo lilimpita
kipa wa Bolton, Jussi Jaaskelainen katika dakika ya 11
na mpira huo kujaa wavuni.
Chelsea iliongeza bao la pili ambalo lilifungwa na
Florent Malouda katika dakika ya 41, ambapo katika
dakika ya 74 Nicolas Anelka alimpa pasi Ramires
ambaye aliipatia Chelsea bao la tatu.
Chelsea ambayo iliichapa Blackburn wiki iliyopita
bado ipo pointi saba nyuma ya vinara wa ligi kuu ya
England, Manchester United  huku ikiwa inashika
nafasi ya nne.
"Didier alitusababisha kuanza vizuri kwa kufunga bao
ambalo ni bora kabisa msimu huu mpaka sasa, kwa
sababu baada ya bao hilo tulijituma sana uwanjani
kwa juhudi zetu zote, ambapo tulifanikiwa
kuwasimamisha Bolton kucheza na hilo lilitusaidia
sisi,"alisema nahodha wa Chelsea John Terry.
Kabla ya mechi hiyo haijanza ilitanguliwa na dakika
moja ya ukimya kuomboleza kifo cha mchezaji wa
zamani wa Bolton na England, Nat Lofthouse
ambaye amefariki mwanzoni mwa mwezi huu.
Katika dakika za mwanzo wa mchezo Bolton iliweza
kutawala, lakini Malouda alipoweza kumnyang'anya
mpira Gretar Steinsson alimpasia Drogba ambaye
alifungua kitabu cha magoli na kufikisha mabao tisa
katika ligi kuu ya England.
"Nilikuwa katika nafasi nzuri, hivyo nilijaribu kuitumia
nafasi hiyo, nilikuwa najiamini kujaribu kupiga shuti lile,
unatakiwa ujaribu  kama unataka kufunga
bao,"alisema Drogba.
Hata hivyo katika mechi hiyo ambayo Chelsea
waliibuka na ushindi, walijikuta katika dakika ya 12
kipa wao Petr Cech kufanya kazi ya ziada kuokoa
mpira wa kichwa kikali ulipigwa na
Matt Taylor ambaye alikuwa akiunganisha krosi
iliyopigwa na  Martin Petrov.
Bolton walishindwa kuhimili kasi ya Chelsea ya
kushambulia kwa kustukiza katika mechi hiyo, huku
Mghana Michael Essien akiweza kuwa kiungo
muhimu kwa upande wa Chelsea.
Mpaka sasa Bolton baada ya kucheza mechi 10
katika ligi kuu ya England imeweza kupata pointi
nane tu hivyo kushika nafasi ya 10 katika ligi hiyo. 
"Tuliwazawadia magoli yote, tulikuwa na nafasi nyingi
kama walizozipata Chelsea, lakini Chelsea walitumia
sisi tulishindwa ndiyo maana Chelsea ni mabingwa
watetezi, ni vigumu kupokea matokea haya, lakini
kuna mambo mawili, kuhuzunika au kuamka asubuhi
na kufanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza, sisi
tutafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza,"alisema
kocha Bolton, Owen Coyle.

 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE