KESI ZA UCHAGUZI KUGHARIMU BIL. 23

Mahakama Kuu

Aziza Masoud

ZAIDI ya Sh23 bilioni zinahitajika ili kusikiliza na kuyatolea maamuzi  mashauri ya kupinga matokeo ya uchaguzi  yaliyofunguliwa kwenye mahakama zote nchini katika kipindi cha mwaka jana.
Fedha hizo zinatarajiwa kutumika kwa gharama za kuwasafirisha majaji na watumishi wengine watakaohusika katika kesi zote za uchaguzi.
Taarifa zilizopatikana ndani ya mahakama zilieleza kuwa katika kipindi cha mwaka jana ambao ulikuwa mwaka wa uchaguzi jumla ya kesi 44 za kupinga matokeo ya uchaguzi zilifunguliwa.
Taarifa hizo zilieleza kesi  hizo zilifunguliwa katika mikoa tofauti nchini ambapo mkoa ambao uliongoza kuwa na kesi nyingi ni  Tabora ambao ulikuwa na kesi tisa ukifuatiwa na Dar es Salaam na Mwanza ambayo yote ilikuwa na idadi sawa ya kesi saba.
Katika Mkoa wa Mtwara kuna kesi tano ikifuatiwa na Mbeya wenye kesi nne na katika Mikoa ya Arusha na Moshi ambayo ina  idadi sawa iliwasilisha ya kesi tatu .
Kwa upande wa Mkoa wa Dodoma na Iringa  zilifunguliwa  mbili kwa kila mkoa wakati Rukwa  na Kagera  zilikuwa kesi mojamoja  huku Tanga na Ruvuma ikiwa haina kesi hatam moja.
Hata ivyo taarifa hizo zilieleza kuwa kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi mashauri ya kupinga matokeo yanapokelewa na kutolewa maamuzi  kwa kipindi cha miaka miwili mara tu   baada ya uchaguzi.
Ilisisitizwa kuwa si vizuri  majaji na wasaidizi wao watakaosikiliza mashauri hayo watoke mahala wanapoishi na kufanyia kazi.
Hivyo basi kwa sababu hiyo mahakama inatakiwa kutoa gharama za kuwasafirisha majaji na wasaidizi wao kwenda sehemu tofauti na walizopo ili kuweza  kusikiliza mashauri   hayo. 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE