SHULE BINAFSI ZATESA KIDATO CHA PILI

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa
Shule binafsi zapeta kidato cha pili Dar   Send to a friend 
Sunday, 23 January 2011 20:37 
0diggsdigg
Exuper Kachenje
MATOKEO ya Mtihani wa Taifa wa kidato cha pili mwaka 2010 Kanda ya Dar es Salaam yametolewa kimya kimya na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, huku shule binafsi zikiongoza na zile za Serikali zikiachwa mbali, Mwananchi limebaini.
Shule za Thomas More, Feza na Lilia Kibo, Canossa, St Joseph Millenium na Pius zimeng'ara katika matokeo hayo Kanda ya Dar es Salaam zikiwa katika kumi bora.
Nyingine zilizo katika kumi bora kwenye kanda hiyo yenye shule 294 ni shule ya sekondari Alpha, Barbro Johnanson na Tusiime.
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa matokeo hayo yametolewa kimya kimya, tangu wiki iliyopita na baadhi ya shule tayari zinajua nafasi zake katika msimamo wa matokeo hayo.
Kwa mujibu wa matokeo hayo ambayo Mwananchi imefanikiwa kuiona nakala yake,  shule za serikali zimeanza kuonekana kuanzia nafasi ya 34 ambayo imeshikwa na sekondari ya Pugu ikifuatiwa na Kisutu nafasi ya 35 ambapo Azania imeshika nafasi ya 37.
Kwa mujibu wa matokeo hayo, sekondari ya Thomas More imeongoza baada ya kupata jumla ya alama 740, ikiwa na wastani wa 82 ambao ni daraja A.
Imefuatiwa na shule za sekondari Feza wavulana na Feza wasichana, ambapo Canossa imekuwa ya nne iliyofuatiwa na St Joseph Millenium na Pius Sekondari.
Sekondari ya Lilian Kibo imeshika nafasi ya saba ikiwa na jumla ya alama 649 ambao ni wastani wa 82 ambapo imepanda kutoka nafasi ya 20 iliyoshika mwaka uliopita hivyo kuonekana imefanya vizuri tofauti na shule nyingine.
Matokeo hayo Kanda ya Dar es Salaam yanaonyesha shule za Kata kuanguka vibaya zikishika nafasi za chini pamoja na kushika mkia.
Matokeo hayo pia yamezitupa mbali shule zenye majina ya watu maarufu ikiwemo Benjamin William Mkapa iliyoshika nafasi ya 50, Mama Salma Kikwete iliyo nafasi ya 75 na Madiba (Nelson Mandela) nafasi ya 63.
Shule ya kata Kibugumo wilayani Temeke imeshika mmkia baada ya kuambulia alama 151 ikiwa na wastani wa jumla ambao ni 17.
Shule hiyo iliambulia alama 6 katika somo la Hisabati, Kiingereza 24 na Kiswahili 25, huku shule nyingine zilizo mkiani juu ya Kibugumo zikiwa ni Temeke Muslim, Emet, Pugu Station na Geoge Washington.
Nyingine ni Mpiji Majohe, Kwetu, Kimbiji na Nguva.
Hata hivyo, matokeo hayo hayana athari kwa wanafunzi kutokana na Serikali kuamua usiwazuie wanafunzi kuendelea na masomo ya kidato cha tatu.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
          
 
Add comment

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE