SITTA,MWAKYEMBE WAIMEGA CCM


Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe


Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki


na Mwandishi wetu
 UPO mpasuko wa wazi ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kama ambavyo vikao na matamko mbalimbali yanayotoka kwenye chama hicho yanavyoonyesha, hasa kuhusu sakata la serikali kulipa mabilioni ya shilingi kwa kampuni ya Dowans.

Baada ya kauli ya Umoja wa Vijana wa CCM juzi kumtaka mwenyekiti wa chama hicho, Jakaya Kikwete, achukue maamuzi magumu kukinusuru chama, hasa kwa kuwachukulia hatua kali vigogo wawili, Waziri wa Ushrikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, na Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, Kamati Kuu ya chama hicho imetoa tamko la onyo kwa vijana hao.

Katibu Mwenezi John Chiligati aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ‘amri’ ya vijana hao kwa Rais Kikwete kwamba awachukulie hatua Sitta na Mwakyembe ni suala la serikali na si la chama.

Alisema kufanya hivyo ni kuingilia mamlaka ya Rais iliyowekwa kwa mujibu wa sheria ambayo hutumika kuongoza nchi na kwamba Kamati Kuu inaiachia serikali kuliangalia hilo.

Huku akisisitiza kwamba tamko la UVCCM ni haki ya kitengo hicho cha chama, alisema Kamati Kuu itawaelimisha zaidi vijana hao na akasisitiza: “Ni lazima maamuzi ya chama yaheshimiwe.”

Alisema maamuzi ya kikao cha Kamati Kuu iliyokutana Januari 20, mwaka huu, imejadili masuala mbalimbali ikiwemo hali ya siasa nchini na kusema kuwa ni lazima serikali iheshimu maamuzi ya mahakama ya kimataifa ya biashara kuhusu mgogoro wake na TANESCO, unaolazimu serikali kuilipa Dowans fidia ya sh 94 bilioni.
Alisema hukumu hiyo ni funzo tosha kwa serikali, hasa katika kuingia mikataba ya miradi ya maendeleo na hata inapotaka kuivunja ni lazima ifuate sheria zilizopo, ikiwa ni pamoja na kufanya makubaliano yenye tija kwa taifa.

“Tunajua hili lililotokea hasa kutokana hukumu ya TANESCO kwa Dowans, tunajua kila Mtanzania ana haki ya kutoa maoni lakini kubwa ni uamuzi wa kisheria na hatuna budi kuuheshimu; kwanza tusubiri uamuzi wa pingamizi lililowekwa Mahakama Kuu ndipo taratibu nyingine zifuatwe na hata tamko la UVCCM ni maoni yao tutakaa nao sisi kama chama na kuwaelekeza taratibu za chama, “ alisema Chiligati.

Alisema TANESCO ilifanya kosa, na Kamati Kuu inaisisitizia serikali umuhimu wa kuzingatia na kuheshimu sheria, ikiwamo maamuzi yaliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Biashara (ICC).

Hata hivyo, alisema pamoja na hukumu hiyo, ni vema serikali ikasubiri uamuzi wa mahakama kuhusu pingamizi lililofunguliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binaadamu (LHRC) juu ya malipo hayo.
Sakata ya Dowans

Chiligati, alisema Kamati Kuu imeona ni vema kuheshimu maamuzi ya Mahakama na hakuna budi kutekeleza hukumu hiyo ila ni busara kwa serikali kutolipa malipo hayo ya bilioni 94 hadi uamuzi wa Mahakama Kuu kuhusu pingamizi lililowekwa na Kituo cha Haki za Binaadamu liamuliwe ndipo taratibu nyingene zifuate kwa mujibu wa sheria

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE