TANZANIA YAKUBALI KUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA UWEKEZAJI AFRIKA

PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TANZANIA imekubali kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Tisa wa Uwekezaji Katika Afrika ambao mwaka huu utalega hasa uwezekaji katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki – Africa Investment Forum 2011 Focusing on East Africa – utakaondaliwa kwa pamoja baina ya Serikali ya Tanzania, Baraza la Biashara la Jumuiya ya Madola (CBC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Msimamo huo wa Tanzania umetangazwa leo, Ijumaa, Januari 21, 2011, na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kufuatia ombi la pamoja la Baraza la Biashara la Jumuiya ya Madola, EAC na Baraza la Biashara la Afrika Mashariki kwa Serikali ya Tanzania.
Rais Kikwete ametangaza msimamo huo wa Tanzania wa kukubali kuwa mwenyeji wa mkutano huo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe kutoka Jumuiya ya Biashara ya Jumuiya ya Madola, ECA, Baraza la Biashara la Afrika Mashariki, Ikulu, Dar Es Salaam. Mkutano huo umepangwa kufanyika Dar es Salaam Aprili 17-19, mwaka huu, 2011.
Ujumbe huo ulioongozwa na Dkt. Mohan Kaul, Mkurugenzi Mkuu wa CBC, uliwashirikisha pia Katibu Mkuu wa EAC, Balozi Juma V Mwapachu na Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la Afrika Mashariki, Bwana Reginald Mengi.
Wengine waliohudhuria mkutano huo ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwezeshaji na Uwekezaji - Dkt. Mary Nagu na Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bwana Emmanuel Ole Naiko.
Mara ya mwisho mkutano wa Africa Investment Forum (AIF) ulifanyika nchini Ghana ambayo iliandaa mkutano wa nane mwaka jana, na Dk. Kaul amemwambia Rais Kikwete kuwa Tanzania imechaguliwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa mwaka huu kwa sababu ya utulivu wake, pamoja na sifa zake za kuleta mageuzi ya kiuchumi na sera nzuri ya uwekezaji.
Mkutano huo wa siku tatu unatarajiwa kuhudhuriwa pia na wakuu wote wa nchi wanachama wa EAC ambao wataombwa kuongoza majadiliano ya jinsi kila nchi inavyoweza kuvutia wawekezaji katika nchi zao.
Mwisho.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
Dar es Salaam.
21 Januari, 2011

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE