WANAFUNZI MAKUMIRA WATAWANYWA KWA MABOMU

Kwa hisani ya tovuti ya Mwananchi
JESHI la polisi mkoani Arusha jana limelazimika kuwatawanya wanafunzi wa chuo kikuu kishiriki cha Tumaini(Makumira) kwa kutumia mabomu ya machozi baada ya wanafunzi hao kugoma kuingia madarasani na kuziba barabara kuu ya Arusha -Moshi kwa mawe na wao kusimama katikati ya  barabara hiyo.
Wanafunzi hao waliokuwa wamebeba mabango yenye ujumbe wa aina tofauti walidai kuwa  chanzo  cha wao kugoma kuingia madarasani ni kutaka kufahamu hatma ya mikopo yao ambayo imecheleweshwa na kuwasababishia kuishi katika mazingira magumu.


Wakizungumza chuoni hapo wanafunzi hao walidai kuwa kwa muda mrefu sasa wamekuwa wakisubiri kutumiwa mikopo hiyo pasipo mafanikio yoyote na kuwasababishia kukosa hata hela kwa matumizi mbalimbali ikiwemo ya chakula.



 "Tunasikitishwa sana na bodi ya mikopo kwa kutucheleweshea mikopo yetu  kwani inatufanya tuishi katika mazingira magumu kiasi kwamba kuna baadhi ya wanafunzi wenzetu wa kike kutokana na hali ngumu ya maisha hapa chuoni wamefikia hatua ya kuuza miili yao ili wapate chochote"alisema mwanafunzi mwingine ambaye hakutaka kutaja jina lake

Wanafunzi hao wameiomba serekali kufanya jitahada ya kuwasaidia wanafunzi hao mikopo ili waweze kujikwamua katika hali hiyo ya umaskini kwani wakilifumbia macho watapoteza vijana wengi ambao wanategemewa kuwa viongozi wa hapo baadaye ukizingatia gonjwa hatari la Ukimwi.


Naye Mkuu wa chuo hicho Joseph Parsalaw alisema kuwa  anashangazwa sana na hatua ambayo wamechukua wanafunzi hao kwa kufanya kitendo cha kuandamana kushinikiza bodi ya mikopo kuwatumia mikopo yao kwani hakijawahi kutokea chuoni hapo.
Alisema kuwa chuo hakikuwa na taarifa zozote za kufanyika kwa mgomo huo na maandamano hayo  na kubainisha kuwa suala la mikopo kwa wanafunzi hao lilikuwa taayari limewasilishwa  na wakati wanafunzi hao wakifanya maandamano hayo wao walikuwa katika kikao wakiyajadili namna ya kulitatua tatizo hilo chuoni hapo

Mkuu huyo aliffanua kuwa  wao kama chuo hawazuii,wala hawatoi mikopo kwa wanafunzi hao bali wanatumia serekali ya wanafunzi ambao inawasilisha wanafunzi hao katika bodi ya mikopo .

Alidai kuwa rais wa wanafunzi chuoni hapa alikwenda katika bodi ya mikopo ambapo alikuta jumla ya wanachuo 642 wameshapatiwa mikopo na 84 bado asilimia za mikopo yao haijulikana huku wengine 136 asilimia zao hazijaonekana katika bodi ya mikopo.

"Uongozi wa chuo haukuwa na taarifa zozote za kufanyika wka mgomo na maandamano hayo ambapo kati wanafunzi  47 tu ndiyo  ambao hawajapata mikopo yao lakini wengine wote zaidi ya 200 tayari wameshapatiwa mikopo"alisema Parsalaw.

Aidha mkuu huyo alikanusha vikali madai ya baadhi ya wanafunzi hao kuwa katika orodha ya majina ya wanafunzi waliopatiwa mikopo kuwa siyo ya wanafunzi wa chuo hicho. .

Alisema wanafunzi hao kwa kuwa wameona wenzao katika vyu vikuu vingine wakiandamana nao wameiga wakidhani ndiyo njia mbadala ya kupata haki yao wayayoidai na kuwasihi kufuata njia sahihi katika kutafuta haki yao. .


Alimalizia  kuwa chuo hakijahusika na tatizo la wanafunzi hao kucheleweshewa mikopo yao na amehaidi kuwa chuo kitaendelea kuwasilaiana na bodi ya mikopo ili kujua hatima ya mikopo hiyo ya wanafunzi hao.


Naye kamanda wa jeshi la polisi mkoani Arusha Thobiasi Andengenye amesema kuwa mpaka sasa jeshi hilo limewashikilia wanafunzi 21 kwa ajili ya mahojiano ya kubaini kiini cha maandamano na  kufanya fujo.

Alisema kuwa jeshi  waliamua kuingilia kati kutokana na kuona wanafunzi hao wamezuia barabara kuu ya  Arusha -moshi kwa muda wa saa moja na kusababisha msongamano mkubwa wa magari  pamoja na kusababisha usumbufu kwa wananchi waishio maeneo hayo pamoja na magari ya pitayo katika barabara hiyo.

Andengenye aliwataak wanafunzi hao kuhakikisha kuwa wanafuata sheria wakati wanapodai haki zao badala ya kufanya maandamano
OOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE