MKUTANO MKUU WA TAMWA

Gladness Munuo na Nasima Haji Chumu ambao ni wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Nchini Tanzania (TAMWA) wakikata keki kwa niaba ya wenzao huku wanachama wengine wakishuhudia  mara baada ya kumalizika kwa mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa mikutano uliopo kwenye ofisi za chama hicho huko Sinza Mori jijini Dar es Salaam

Picha no. 6 Baadhi ya wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Nchini Tanzania (TAMWA) wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa  wakati wa  mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa mikutano uliopo kwenye ofisi za chama hicho huko Sinza Mori jijini Dar es Salaam.
Picha na Anna Nkinda -Maelezo


Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Nchini Tanzania (TAMWA) Ananilea Nkya akiwaeleza  wanachama wa chama hicho (hawapo pichani) kuhusu mafanikio waliyoyapata kwa mwaka wa 2010 wakati wa mkutano mkuu uliofanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo katika ofisi za chama hicho huko Sinza Mori jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mzuri Issa ambaye ni mratibu wa TAMWA Zanzibar na kushoto ni Gladness Munuo.

Ichikaeli Maro (katikati) akipokea zawadi ya kupongezwa kwa kuteuliwa kushika nafasi ya kuwa mhariri  msaidizi wa habari wa magazeti ya Daly News weekend ambayo ni Daily News na Sunday News kutoka kwa Fatma Alloo ambaye ni mwanachama  na miongoni mwa waanzilishi  wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Nchini Tanzania (TAMWA) (kulia) wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika hivi karibuni katika ofisi za chama hicho huko Sinza Mori jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Maryam Hamdani ambaye ni mwanachama wa chama hicho.

Betty Mkwasa (kulia)  ambaye ni Mwanachama  wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Nchini Tanzania (TAMWA) na  Mkuu wa wilaya ya Bahi  akipokea  zawadi ya kumpongeza kwa kupata tuzo ya mwanamke aliyefanikiwa katika mambo ya mawasiliano kwa mwaka 2008 kutoka kwa Maryam Hamdani ambaye ni mwanachama wa chama hicho wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika hivi karibuni huko Sinza Mori jijini Dar es Salaam

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE

MAKALLA ASHANGILIWA BUNGENI

NCHIMBI AFUNGUA KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AKARIBISHWA KIMILA NYUMBANI RUVUMA