BABU WA LOLIONDO AFIWA NA MWANAYE


Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Ngorongoro, wakiwa nyumbani kwa mchungaji Ambilikile Mwasapila (kushoto), wakimpa pole kutokana na kifo cha Jackson Mwasapila(43), kilichotokea katika hopitali ya Wilaya ya Babati Mkoani Manyara jana. Picha na mussa juma

MCHUNGAJI Ambilikile Mwasapila anayetoa tiba ya magonjwa sugu huko Samunge, Loliondo amefiwa na mtoto wake wa kiume jana. Kutokana na msiba huo, Serikali imesitisha tena tiba anayotoa hadi Ijumaa.
Habari zilizopatikana kijijini hapo jana zimeeleza kuwa mtoto huyo, Jackson Mwasapila (43), alifariki dunia jana asubuhi, nyumbani kwake wilayani Babati, Mkoa wa Manyara.
Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali aliliambia gazeti hili jana kuwa kutokana na msiba huo, Mchungaji Mwasapila atasitisha tiba kuanzia leo jioni.Mkuu huyo wa Wilaya alifika Samunge jana hiyo hiyo akiwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, kumpa pole mchungaji huyo.
"Tunapenda kutangaza rasmi kuwa huduma zitasitishwa hadi Ijumaa na tunaomba watu walio mbali wasije hadi Ijumaa," alisema Lali.Alisema Serikali itashiriki msiba huo na inajiandaa kutoa msaada wa kumpeleka Mchungaji Mwasapila, Babati kushiriki msiba huo.
Mchungaji azungumziakilichomsibu mwanaye Akizungumza na gazeti hili kijijini hapo jana, Mchungaji Mwasapila alisema mtoto wake huyo alifariki jana saa 5:00 asubuhi katika Hospitali ya Wilaya ya Babati baada ya kuugua malaria ghafla.
"Taarifa ambazo nimezipata ni kuwa Jackson alikuwa anasumbuliwa na kichwa na baada ya kufikishwa hospitali, alifariki dunia," alisema Mchungaji Mwasapila.Mchungaji huyo, alisema Jackson ni mtoto wake wa tatu kati ya sita alionao.
Wagonjwa wampa poleBaadhi ya wagonjwa waliokwenda Samunge jana kupata tiba, walitoa salamu za rambirambi kwa Mchungaji Mwasapila kutokana na msiba huo.Hata hivyo, wakati wagonjwa hao wakimpa pole, mchungaji huyo alikuwa akiendelea kuwapa dawa kama kawaida.
Mchungaji Mwasapila alisema ameamua kuendelea na kutoa tiba kwa wagonjwa hao ili kuwasaidia watu ambao tayari walikuwa wamefika Samunge na wengine watakaofika leo. "Kesho (leo) jioni nitafunga na kuelekea Babati kwa ajili ya msiba wa mtoto wangu na kama alivyosema mkuu wa wilaya, tutaendelea na tiba Ijumaa," alisema Mchungaji Mwasapila.
Foleni yapungua Samunge Katika hatua nyingine, msongamano wa magari yaliyoanza kwenda kijijini hapo baada ya Pasaka umeanza kupungua. Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa mengi ya magari hayo, yalikuwa yamebeba wagonjwa kutoka Kenya.
Serikali ilishafungua vizuizi vya Bunda, Mto wa Mbu, Londigo na Loliondo mjini vilivyokuwa vimefungwa kwa muda wakati wa sherehe za Pasaka.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE