CAG AIBUA UOZO AJIRA TANAPA

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh.


WATUMISHI 181 wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa), wameajiriwa kinyume cha taratibu za ajira.
Ajira hizo zisizofuata taratibu ndani ya shirika hilo, zimebanika wakati wa ukaguzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh.
Kwa mujibu wa Utouh, Tanapa ni mfano wa mashirika mbalimbali ya umma yanayotoa ajira za watumishi kwenye sekta mbalimbali kinyume cha taratibu.
Utouh anabainisha kwenye uchambuzi wa usimamizi wa raslimali watu katika mashirika mbalimbali ya umma, kuna mashirika ambayo ajira za kazi zilifanywa bila kufuata taratibu za uwazi.
Anabainisha taratibu hizo zinazokiukwa na mashirika hayo wakati wa ajira kuwa, ni kutangaza nafasi zilizo wazi, jambo ambalo linawanyima watu wengi nafasi ya kushindana.
“Mfano mzuri ulibainika Tanapa ambapo menejimenti ilitangaza nafasi 19 za kazi kuwa uwazi, lakini kufikia mwisho mwa zoezi la uajiri, wafanyakazi 32 zaidi waliajiriwa;“Uchambuzi zaidi ulibaini kuwa wafanyakazi walioajiriwa na Tanapa mwaka huu wa ukaguzi bila nafasi zake kutangazwa ni 181” anasema Utouh.
Licha ya ukiukaji taratibu za ajira katika mashirika ya umma, CAG amebainisha ukiukaji mkubwa wa sheria na haki za wafanyakazi.Miongoni mwa kasoro hizo za ukiukaji sheria na haki za wafanyakazi uliobainishwa, ni kuchelewa kulipa mishahara na malipo ya mishahara chini ya kima cha chini
Taarifa hiyo imebainisha kuwa, uchambuzi wa usimamizi wa raslimali watu juu ya suala la ulipaji mishahara, baadhi ya mashirika ya umma hayatoi umuhimu wa kutosha kuhusu haki ya wafanyakazi kulipwa mishahara.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, baadhi ya mashirika yamekuwa hawalipwi mishahara yao kwa wakati, huku mengine yakiwalipa wafanyakazi wao chini ya kima cha chini cha mshahara.
Shirika lingine ambalo halikuwalipa wafanyakazi wake mishahara, ni Tamko Kibaha ukaguzi huo umebaini kuwa wafanyakazi saba wa zamani, hawakulipwa mishahara yao ya jumla ya Sh2.6 millioni.
Pia, Nyanza Glass Works Limited na Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), kuwa yanawalipa wafanyakazi wake mishahara chini ya kima cha chini cha mishahara.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE