FOLENI BAADA YA BENKI KUFUNGULIWA IVORY COAST



Maelfu ya raia wa Ivory Coast wamepanga foleni kutoa pesa na kupokea mishahara iliyocheleweshwa kufuatia benki nchini humo kufunguliwa tena baada ya kufungwa kwa wiki 10.
Kufungwa kwa benki hizo kulitokana na jaribio la aliyekuwa Rais Laurent Gbagbo kung'ang'ania madarakani baada ya uchaguzi wenye utata.
Kufunguliwa tena kwa mfumo wa benki ni hatua ya kufufua uchumi wa nchi inayoongoza kwa uzalishaji wa kakao duniani.
Serikali ya rais mpya Alassane Ouattara imeahidi kulipa mishahara ya miezi miwili kwa sekta za umma.
Raia wa nchi hiyo walitaarifiwa kwa kipindi kifupi juu ya kufungwa kwa benki hizo mwezi Februari, wakiacha maelfu wakihangaika kumudu maisha yao bila mishahara, mafao ya uzeeni na akiba.
Mteja mmoja aliyekuwa kwenye foleni nje ya benki iliyokuwa kwenye mji mkuu Abidjan, alisema alikuwa akisubiri tangu mapema asubuhi kutoa pesa za kutosha kwa ajili ya kulisha familia yake.
Alisema, "Ntaitunza familia yangu iliyoteseka kwa takriban miezi miwili bila ya kuwa na chakula cha kutosha. Ntawatunza watoto na kuhakikisha wanarudi shuleni. "
Sekta ya biashara nayo imekwama kufanya kazi kwa ufanisi na biashara kuu ya kakao, inabaki ikisuasua.
Mwandishi wa BBC John James aliyopo mjini humo, japo vikwazo vimeondolewa, wafanyabiashara wanahitaji akaunti zao za benki kabla ya kulipa ushuru wa forodha.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE