KUBORONGA KWA ARSENAL WENGER LAWAMANI

ARSENE WENGER
Arsenal kuboronga, Wenger abeba lawamaMeneja wa Arsenal Arsene Wenger, amesema alaumiwe kutokana na timu yake kufanya vibaya msimu huu, baada ya kufungwa mabao 2-1 na Bolton hali iliyosababisha kupoteza matumaini ya kutwaa ubingwa.

Arsenal kwa sasa ipo nyuma ya vinara wa Ligi Kuu ya England, Manchester United kwa pointi tisa, ikiwa imesalia michezo minne kabla ligi haijamalizika msimu huu.
Iwapo Manchester United watashinda siku ya Jumapili katika uwanja wa Emirates, itakuwa na maana Arsenal itaendelea kukosa kombe kwa msimu wa sita mfululizo.
"Wachezaji walicheza kwa kiwango cha juu kwa msimu mzima. Iwapo kutakuwa na mtu wa kubeba lawama, ni mimi, alisema Wenger.
Wenger amekiri baada ya kupoteza mchezo katika uwanja wa Reebok, kwamba nafasi ya timu yake kushinda ubingwa msimu huu imeyeyuka.
"Inatupasa kucheza kwa nguvu zetu zote hadi mchezo wa mwisho, lakini hapana shaka nafasi yetu ni finyu kwa sasa," aliongeza.
Arsenal katika mchezo dhidi ya Bolton walipata nafasi nyingi kipindi cha pili kuweza kushinda mchezo huo, nyingi zikipotezwa na Samir Nasri, ambaye mara mbili alishindwa kuweka mpira wa wavuni akiwa katika nafasi nzuri.
"Ni vigumu kupokea namna tulivyopoteza mchezo," alisema Wenger.
"Tulikuwa na nafasi nzuri kushinda. Hatukutumia nafasi hizo na tulikuwa wadhaifu sana kuokoa mipira ya kona.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE