MWANAMFALME WA UINGEREZA APATA JIKO

Mwana mfalme William akimpiga busu Kate
Mwana mfalme William akifungishwa ndoa na Aksofu Rowan William katika kanisa la Westminster Abbey jijini London.

Mwana mfalme wa Uingereza, Prince William na Kate
Middleton wamefunga ndoa katika kanisa la
Westminster Abbey jijini London.


Takriban wageni 1,900 walishuhudia tukio hilo ndani
ya kanisa, na mamilioni wakifuatilia majumbani mwao
kwa njia ya televisheni.


Maharusi hao walishangiliwa na maelfu ya watu
waliojipanga barabarani kuelekea kasri ya Buckingham
Palace ambako Malkia amewaandalia karamu wageni
650.


Wana ndoa hao wapya walitumia gari liliovutwa na
farasi la muundo wa mwaka 1902 ambalo lilitumiwa
na wazazi wake Prince William wakati wa ndoa yao
mwaka 1981.


Maharusi hao baadaye walijitokeza kwenye roshani ya
kasri ya Buckingham na kuwasalimu maelfu ya watu
waliokwenda kuwasherehekea.


Baada ya kulishana viapo vya ndoa Askofu mkuu wa
Canterbury, Rowan Williams, aliwanadi rasmi kuwa
"mume na mke".


Kuanzia sasa maharusi hawa watajulikana rasmi kama
Duke na Duchess wa Cambridge.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE