RAC, MEYA WAZOMEWA MSIBANI

KATIBU Tawala Msaidizi Mkoa wa Shinyanga, William Nsanzugwanko na Naibu meya wa manispaa hiyo, Grace Machiya, wamejikuta katika wakati mgumu baada ya kuzomewa na wananchi walipoitwa kutoa salamu za rambirambi kwenye mazishi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani hapa, Philipo Shelembi.

Shelembi, pia alikuwa Diwani wa Kata ya Masekelo,Manispaa ya Shinyanga na mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema Taifa, alifariki juzi kutokana na shinikizo la moyo na kiharusi.

Baada ya kuitwa viongozi hao kutoa salamu zao, wananchi walipiga kelele huku wakidai kuwa, hawamtaki mkuu wa mkoa kwa sababu ni mwanachama wa CCM, ambao wote ni mafisadi waliomchakachua Shelembi kwenye uchaguzi mkuu mwaka jana.

Nsanzugwanko alikuwa anamwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Brigedia Jenerali Dk Yohana Balele. Shelembi alikuwa mgombea ubunge wa Chadema Jimbo la Shinyanga, alishindwa kwa tofauti ya kura moja na mwenzake wa CCM, Steven Masele.

Hata hivyo, wakati kelele hizo zikiendelea, Nsanzugwanko tayari alikuwa amepanda jukwaani, lakini kelele zilizidi zikitaka ashuke na kwamba, angeendelea wangempopoa mawe huku wengine wakizomea.

“Hatumtaki mkuu wa mkoa na meya wasimame jukwaani hapo, wote ni CCM walewale mafisadi, ndio waliyemchakachua mbunge wetu, Shelembi Mwanabyula, aliyekuwa mtetezi wa wanyonge, wakikatalia jukwaani tutawaponda mawe, ” wasikika wakisema wananchi hau kwa kupaza sauti na kuongeza:"Tumechoshwa na mafisadi wa kutuchakachua, wametuchakachua kura tuwaruhusu wapande jukwaani, hatuwataki waongee jukwaani watuache tuna majonzi ya kuondokewa na mbunge wetu tuliyemchaguwa ."

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alisema Shelembi alikuwa mtetea haki ya Watanzania wote, mwadilifu aliyepigania haki ya wanyonge huku akisisitiza: “Tutaendelea kudai haki, tutaandamana na polisi hilo mlijue.”

Mbowe alisema kuanzia Mei 4, wataanza maandamano ya amani nchi nzima watarudi Shinyanga hadi kieleweke.

“Siku zote gamba hatuliogopi na haliwezi kupunguza sumu ya nyoka,” alisema Mbowe na kuongeza:“Nia yetu sio kulipiza kisasi ni kuongoza Watanzania, kesi aliifungua marehemu Shelembi na leo hatunaye tena tuwe na subira tunakwenda kukaa na viongozi tutawajulisha tutakavyoamua.”

Mazishi hayo yalihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, Makamu Mwenyekiti Chadema Zanzibar na viongozi mbalimbali. Heshima za mwisho zilitolewa uwanja wa ShyCom.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE