SUMATRA YAADHIBU MABASI YALIYOPANDISHA NAULI PASAKA

MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri Nchi Kavu na Majini (Sumatra), imekusanya Sh 1.75 milioni kutokana na faini walizowatoza wenye magari yaliyopandisha nauli wakati wa Sikukuu ya Pasaka.

Akizungumza na Mwananchi jana kwa njia ya simu Ofisa Uhusiano wa Sumatra, David Mziray alisema fedha hizo zimetokana na kukamatwa kwa magari ya abiria ambayo yanafanya safari za mikoani.

“ Tumekamata magari tisa yakiwemo saba yanayo fanya safari za Kilimanjaro na mawili ya Lushoto na kila basi moja tumelitoza faini ya Sh 250,000 pamoja na kuwapa adhabu ya kuchukua vibali vyao vya usafirishaji,” alisema Mziray.

Mziray alisema walifanya hivyo ili iwe fundisho kwa vyombo vingine vya usafiri vyenye tabia kama hiyo ya kujipandishia nauli kiholela bila kufuata utaratibu uliowekwa na mamlaka.
“ Adhabu hii tuliyoitoa itakuwa fundisho kwa vyombo vingine vyenye tabia ya kujipandishia nauli bila kufuata utaratibu hali ambayo inaleta usumbufu kwa watumiaji,” alifafanua.

Mziray aliongeza kusema kwa pamoja na kuwatoza faini wamiliki wa mabasi hayo wamefuta vibali 11 vya kusafirisha abiria kwa mabasi yaliyohusika kupandisha nauli.

“Tumefuta vibali 11 vya magari ambayo yalihusika kupandisha nauli bila kufuata utaratibu tumelazimika kufanya hivyo kwa sababu walisababisha usumbufu mkubwa kwa abiria.” alisema Mziray.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE