UN YAKERWA NA MAUAJI SYRIA

Jeshi limewaua mamia ya watu wanaoandamana kupinga utawala nchini SyriaWanadiplomasia katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa wanadadisi mswada unaolaani ghasia zinazoendelea nchini Syria.

Mswada huo uliopendekezwa na Uingereza, Ufaransa, Ujerumani na Ureno unataka serikali ikomeshe mashambulio dhidi ya raia.

Wanachama hao pia wanaunga mkono Katibu Mkuu Ban Ki Moon, ambaye amependekeza uchunguzi ufanyike kuhusu mauaji ya mamia ya waandamanaji wiki chache zilizopita.

Nchi zilizopendekeza mswada huo, zinamatumaini kuwa wanachama wa baraza la usalama watakubaliana kwa haraka kuhusu mswada huo na kuupitisha katika mkutano wao hii leo.

Baraza hilo limekuwa kimya kuhusu hali tete ilioko katika nchi za kiarabu ila tuu Libya. Wiki iliopita wanachama walishindwa kukubaliana kuhusu mzozo unaoendelea nchini Yemen.

Nayo serikali ya Marekani huenda ikaiwekea Syria vikwazo kama ishara kuwa inakerwa na hatua za serikali hiyo dhidi ya raia wanaoandamana.

Vikwazo hivyo huenda vikawalenga vigogo wa serikali na hata kuharamisha biashara kati ya Syria na Marekani.

Serikali ya Rais Obama imelaumiwa sana kwa jinsi ilivyoshughulikia mzozo unaoendelea Syria ikilinganishwa na hatua za serikali yake nchini Libya.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI