UNITED YAICHAPA SCHALKE 2-0

Giggs amekuwa mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kufunga goli katika michuano hii


United yaichapa Schalke 2-0Manchester United imepiga hatua kubwa kuelekea katika fainali ya Klabu Bingwa Ulaya, baada ya kuifunga Schalke katika nusu fainali ya kwanza nchini Ujerumani.

United wangeweza kufunga mabao mengi kabla ya mapumziko, kama sio uhodari wa kipa wa Schalke, Manuel Neuer.


Hata hivyo United walipata bao la kwanza katika kipindi cha pili, baada ya Wayne Rooney kupenyeza pasi wa Ryan Giggs. Rooney baadaye alipachika bao la pili baada ya kupata pasi kutoka kwa Javier Hernandez.


United itaikaribisha Schalke kwenye uwanja wa Old Trafford, Jumatano tarehe 4 mwezi Mei, kwa ajili ya mchezo wa pili wa nusu fainali.


Iwapo watadhibiti ushindi wao, United itawakilisha soka ya England katika Fainali ya Klabu Bingwa Ulaya itakayochezwa kwenye uwanja wa Wembley.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE