Mwakilishi wa Inspekta Jenerali wa Polisi, Kamishna Paul Chagonja (kushoto) akipigiana saluti na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya simu ya Airtel, Chiruyi Walingo baada ya kukabidhiwa msaada wa simu 60 na modemu 60 kwa ajili ya matumizi ya mawasiliano ya jeshi hilo. Hafla hiyo imefanyika leo Makao Makuu ya Jeshi la Polisi.
CHAMA KIPYA CHA WALIMU WAMUOMBA RAIS SAMIA AINGILE KATI MAKATO YA WANACHAMA WAO
Chama cha Kulinda na Kuwatetea Walimu Tanzania (CHAKUWAHATA) kimemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kuingilia kati sakata la baadhi ya wakurugenzi kukiuka sheria ya kuwaruhusu walimu kujiunga na chama hicho hivyo makato ya fedha za mishahara yao kuingizwa kwenye chama hicho. Ombi hilo limetolewa na Mwenyekiti wa chama hicho, Emmanuel Herman alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari wakati wa Mkutano Mkuu wao unaofanyika jijini Dodoma. Walimu ambao ni wajumbe wa Mkutano Mkuu wa chama hicho wakiwa katika mkutano wa kupitia upya rasimu ya katiba ili ieendane na wakati.
Comments