NAIBU WAZIRI WA UTAMADUNI WA CHINA ATINGA BUNGENI


Waziri Mkuu Mizengo Pinga akiangalia zawadi ya chombo cha kuwekea sukari aliyopewa na Naibu waziri wa Utamaduni wa China, Zhao Shaohua wakati naibu waziri huyo alipomtembelea ofisini kwake jana mjini Dodoma. Zhao pamoja na ujumbe wake wapo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku nne ikiwa na malengo ya kuimarisha mahusiano ya kiutamaduni baina ya Tanzania na China.








Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Utamaduni, Anjela Ngovi akimvalisha kanga Naibu Waziri wa Utamaduni wa China, Zhao Shaohua wakati naibu waziri huyo alipotembelea mjini Dodoma jana, kwa ajili ya kuonana na viongozi wa Serikali huku Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Emmanuel Nchimbi (katikati) na Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni, Prof. Helmasi Mwansoko (kulia) wakishuhudia.






Naibu waziri wa Utamaduni wa China Zhao Shaohua akiangalia ngoma ya kabila la kisukuma iliyokuwa inachezwa na kikundi cha ngoma cha Mwinamila cha mjini Dodoma, wakati naibu waziri huyo alipowasili mjini Dodoma










Naibu Waziri wa Utamaduni wa China, Zhao Shaohua akiangalia zawadi ya picha ya pundamilia aliyopewa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinga wakati naibu waziri huyo alipomtembelea ofisini kwake jana leo mjini Dodoma.



Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Emmanuel Nchimbi (kulia) akisalimiana na Naibu Waziri wa Utamaduni wa China, Zhao Shaohua (katikati) katika Uwanja wa Ndege wa mjini Dodoma,Kulia ni Zhao Haisheng aliyeambatana na ujumbe huo.
(PICHA ZOTE NA ANNA NKINDA-MAELEZO)

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE

MONGELLA AKABIDHIWA ‘MIKOBA’ RASMI YA NAIBU KATIBU MKUU CCM BARA*

NCHIMBI AFUNGUA KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE

DKT NCHIMBI AKARIBISHWA KIMILA NYUMBANI RUVUMA