WABUNGE TUNDU LISSU, LEMA NA MSIGWA WA CHADEMA WATIMULIWA BUNGENI LEO



Naibu Spika Job Ndugai akiwaamuru wabunge wa CHADEMA Tundu Lissu, Mchungaji Peter Msigwa na Godbless Lema kutoka ndani ya Bunge leo mara baada ya wabunge hao kuvunja kanuni ya Bunge ya kuongea bila ruhusa ya Naibu Spika



Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Shamsi Vuai Nahodha akisoma bajeti ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo Bungeni mjini Dodoma leo kwa mwaka wa fedha 2011/2012..







Godbless Lema ambaye ni msemaji mkuu wa kambi ya upinzani kuhusu wizara ya mambo ya ndani ya Nchi akisoma makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2011/2012.
Picha na Anna Nkinda - Maelezo







Askari Polisi wa Bunge wakiwasindikiza wabunge wa CHADEMA Tundu Lissu (kulia) Mchungaji Peter Msigwa (kushoto) na Godbless Lema (wa pili kushoto) ili waondoke nje ya viwanja vya Bunge mara baada ya Naibu Spika Job Ndugai (hayupo pichani) kuwaamuru watoke ndani ya Bunge leo baada ya wabunge hao kuvunja kanuni za Bunge za kuongea bila ruhusa ya Naibu Spika. Wa pili kulia ni Mbunge wa jimbo la Ubungo John Mnyika akiwasindikiza wabunge wenzake.










Gari lililowabeba wabunge wa CHADEMA Tundu Lissu, Mchungaji Peter Msigwa na Godbless Lema likiondoka nje ya viwanja vya Bunge mara baada ya Naibu Spika Job Ndugai (hayupo pichani) kuwaamuru wabunge hao watoke ndani ya Bunge leo baada ya wabunge hao kuvunja kanuni za Bunge za kuongea bila ruhusa ya Naibu Spika.







Askari Polisi wa Bunge wakihakikisha kuwa gari lililowabeba wabunge wa CHADEMA Tundu Lissu, Mchungaji Peter Msigwa na Godbless Lema linaondoka nje ya viwanja vya Bunge mara baada ya Naibu Spika Job Ndugai kuwaamuru watoke ndani ya Bunge leo baada ya wabunge hao kuvunja kanuni za Bunge za kuongea bila ruhusa ya Naibu Spika.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE

MONGELLA AKABIDHIWA ‘MIKOBA’ RASMI YA NAIBU KATIBU MKUU CCM BARA*

NCHIMBI AFUNGUA KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE

DKT NCHIMBI AKARIBISHWA KIMILA NYUMBANI RUVUMA