MATEKA 50,000 WASAKWA LIBYA


Waasi wa Libya wanasema wana wasiwasi na hatma ya maelfu ya wafungwa ambao walikuwa wakishikiliwa na utawala wa Gaddafi.

Waasi wasaka nyumba ya wafuasi wa Gaddafi

Msemaji wa kijeshi wa waasi Kanali Ahmed Omar Bani amesema watu wapatao elfu 50 waliokamatwa miezi ya karibuni hawajulikani walipo.

Waasi wanaamnini kuwa wafungwa hao huenda wanashikiliwa katika maghala ya kijeshi yaliyoko chini ya ardhi, ambayo yametelekezwa.

Vikundi vya kutetea haki za binadamu vina ushahidi kwamba watu wengi wameuawa karibu na magereza, lakini Kanali Bani hajamshutumu yeyote kwa mauaji ya wafungwa hao.

"Idadi ya watu waliokamatwa kwa miezi kadha iliyopita inakadiriwa kuwa kati ya 57,000 na 60,000," amesema katika mkutano wa waandishi wa habari mjini Benghazi."Mpaka sasa, Kati ya wafungwa 10,000 na 11,000 wameachiliwa huru... wengine wako wapi?"

Kanali Bani ameomba kwa yeyote mwenye taarifa kuhusu wafungwa hao kujitokeza, na amesema itakuwa jambo la kutisha iwapo wameuawa.

kuna hofu kuwa maelfu ya wateka wangali wanashikiliwa katika jela lililojengwa chini ya ardhi ambako inasaidikiwa kuwa wamekimbiwa na majeshi ya Kanali Gaddafi wakati waasi walipoingia Tripoli na kuuteka nyara.

Kinachoendelea kwa wakati huu ni pilka pilka za kuwatafuta mateka hao ambao hawajulikano waliko ili waachwe huru.

Al-Megrahi

wakati huo huo viongozi waasi wamesema hawana nia yakumrudisha Abdel Basset al-Megrahi ambaye mwaka 1988 alifungwa jela kwa kulipuwa ndege ya Lockerbie katika anga ya Scotland.

Megrahi aliachiliwa mapema kutika jela miaka miwili iliyopita baada ya madaktari kudai anakaribia kufariki kwani ana miezi michache tu ya kuishi . kuachiliwa kwake kulipingwa na wengi.

Lakini hivi majuzi kumekuwa na shinikozo za kumtaka Megrahi arudishwe uingereza au akafunguliwe amshitaka upya nchini Marekani.

Na shirika la harabi la CNN limemkuta bwana huyo katika jumba la kifahari viungani mwa mji wa Tripoli lakini akiwa mahututi chini ya uangalizi wa familia yake.

Mtumie rafiki
Toleo la kuchapisha

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE