Na Mwandishi Maalum, Zanzibar. Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete, amepongeza kasi ya maendeleo yanayofanyika Zanzibar chini ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Mwinyi na kusisitiza kuwa mafanikio hayo, ambayo yanapaswa kupongezwa na kuenziwa. Dk. Kikwete ametoa sifa hizo, wakati akihutubia jana, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kituo kipya cha Afya Kizimkazi, katika Wilaya ya Kusini Unguja, ambao ni moja ya matukio katika kusherehekea miaka 61 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, ambayo kilele chake kitakuwa Januari 12, 2025. Dk. Kikwete alibainisha kuwa kituo hicho cha kisasa kina uwezo mkubwa wa uchunguzi wa maradhi na tiba, hivyo ni mkombozi wa huduma za afya kwa wakazi wa Kizimkazi na maeneo jirani. Alihimiza umuhimu wa kutunza majengo na vifaa vya kituo hicho ili kuhakikisha huduma hizi za thamani zinadumu kwa muda mrefu."Tukitunze kituo kidumu; ni chetu, ni mali yetu, ni kwa ajili yetu," alisisitiza Dkt. Kikwete. Rais Mstaafu aliambatana na...
Comments