WENGER AUMIZWA NA KIPIGO CHA MABAO 8-2


Arsene Wenger amesema ameaibishwa kwa kuzabwa mabao 8-2 dhidi ya mahasimu wao wakubwa Manchester United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England

Wayne Rooney alifunga mabao matatu katika mechi hiyo ikiwa ni mara yake ya sita kupachika mabao matatu katika mechi moja kwenye uwanja wa Old Trafford huku Manchester United kwa ushindi huo wakikamata usukani wa Ligi hiyo na kumuacha Wenger akiendelea kukabiliwa na mzozo unaokuwa katika klabu ya Arsenal.

"Bila shaka unajihisi kuabishwa unapofungwa mabao manane," alisema meneja huyo wa Arsenal. "Ilikuwa siku mbaya sana."

Wenger amesisitiza ni mapema mno kusema kama sera yake ya uhamisho imeingia dosari kufuatia kuondoka kwa Cesc Fabregas na Samir Nasri na kukosa kiungo wa kuchukua nafasi zao.

Lakini hivi sasa anakabiliwa na kibarua cha kusajili wachezaji kabla ya dirisha la usajili halijafungwa siku ya Jumatano saa tano usiku.

Wenger, ambaye amesisitiza hatang'atuka, anatarajiwa kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Monaco, ambaye pia ni nahodha wa timu ya taifa ya Korea Kusini Park Chu-Young kabla muda wa usajili haujamalizika.

Pia anataka kusajili mlinzi wa kati na kiungo na Arsenal huenda ikarejea tena mbio za kumsajili mlinzi wa kati wa Bolton, Gary Cahill. Maombi yao mara ya kwanza yalitupwa.

Wenger, ambaye alianza kuwa meneja wa Arsenal mwezi wa Oktoba mwaka 1996, ameongeza kusema: "Hatuna budi kutafuta wachezaji wanaofaa na iwapo tutawapata tutawasajili. Pesa tunazo na iwapo tutawapata watakaoimarisha kikosi chetu tutafanya hivyo. Iwapo hatutafanya hivyo, basi itakuwa hatujawapata wachezaji hao wanaotufaa.

Baada ya Arsenal kufungwa vibaya mabao 8-0 mwaka 1896 ugenini na timu ya Loughborough Town katika ligi ya daraja la pili, Wenger ameongeza: "nahisi kufungwa huku kumetokana na hali maalum.

"Wachezaji wetu wengi hawachezi na tumecheza mechi tano tu. Tulichoka mwishoni lakini wachezaji wetu wanane muhimu hawakucheza."

Meneja wa Manchester United Ferguson alitoa maneno ya kufariji akisema: "Tunaishi katika dunia iliyojaa kubeuana na vyombo vya habari vya habari vipo katika mashindano ya kutojali na kuwa tayari kumalizana.

"Ni vigumu kuelewa kwa wakati huu, lakini kazi iliyofanyika miaka 15 iliyopita sasa inaonekana ni ya ajabu sana.

"Alianzisha aina ya soka ya kipekee na mtindo wa usakataji soka wa aina yake na akachukua wachezaji wanaovutia kiuchezaji na pia amefanikiwa kuuza vizuri wachezaji. Hilo naliheshimu."

Nahodha wa Arsenal Robin van Persie, ambaye alikosa kufunga mkwaju wa penalti uliookolewa na mlinda mlango wa United wakati Gunners walipokuwa nyuma kwa bao 1-0, amekiri timu yake haina budi kuimarika kabla ya mchezo ujao wa ligi utakaofanyika Emirates dhidi ya Swansea tarehe 10 mwezi wa Septemba.

"Hatuna budi kurudi katika mstari," alisema mshambuliaji huyo. "Tutakabiliana na Swansea katika wiki mbili zijazo, ambao ni wapinzani wazuri na nausubiri kwa hamu mpambano huo.

"Sidhani kama tunaweza kujificha nyuma ya kivuli cha majeruhi ama kusimamishwa wachezaji. Hakuna kisingizio. Na wao wanao majeruhi pia, hii ni soka."

Mlinzi wa zamani wa Arsenal Lee Dixon amesema Gunners tayari hawakupewa nafasi ya kutwaa ubingwa, lakini akasisitiza Wenger bado ni mtu anayefaa kwa kazi hiyo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE