WANA MISENYI WAKUTANA DAR KUJADILI MAENDELEO

Mbunge wa Jimbo la Nkenge, Mkoani Kagera, Asumpta Mshama akielezea mikakati ya wenyeji wa Wilaya ya Misenyi wanayoifanya kuboresha masuala ya Elimu, Afya na Uchumi kwa ujumla wilayani humo. Alikuwa anazungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa wakazi wa Dar es Salaam wenyeji wa wilaya hiyo, kupitia Mfuko wa Maendeleo wa Misenyi, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Kulia ni Mwenyekiti wa Mfuko huo,Profesa Wenceslaus Kilama.
Baadhi ya wakazi wakiwa katika mkutano huo uliofanyika katika Hoteli ya Picolo, Msasani Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Mfuko wa Maendeleo wa Wilaya ya Misenyi,Profesa Wenceslaus Kilama akitoa maneno ya ufunguzi wa mkutano wa wana Misenyi wa kujadili maendeleo ya wilaya hiyo.
WanaMisenyi wakifurahia jambo wakati wa mkutano huo
Viongozi wa Mfuko huo, wakiingia kwenye mkutano huo. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Misenyi, Kanali msitaafu Issa Njiku, Mbunge wa Nkenge, Asumpta Mshama, Makamu Mwenyekiti wa Mfuko huo, Godfrey Kamukaya na Mwenyekiti wa Mfuko huo, Profesa Wenceslaus Kilama.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI