ARSENAL YAONDOLEWA FA CUP

Arsenal, kwa mwaka wa saba, inaelekea msimu huu utakwisha pasipo kupata ubingwa katika mashindano yoyote, baada ya Jumamosi kufungwa magoli 2-0 katika uwanja wa ugenini wa Stadium of Light dhidi ya Sunderland, katika mechi ya raundi ya tano ya Kombe la FA.

Arsenal, ikiwa katika nafasi ya nne katika ligi kuu ya Premier ya England, na kukiwa na uwezekano mkubwa wa kuondolewa katika ligi ya mabingwa barani Ulaya, inaelekea huu sio mwaka wao wa kupata chochote.

Kieran Richardson aliandikisha bao la kwanza la Sunderland.

Arsenal walijaribu kupata bao la kusawazisha, lakini mkwaju wa Sebastian Larsson ulielekezwa wavuni na mchezaji wa Arsenal, Alex Oxlade-Chamberlain, akimfunga kipa wake mwenye na kuipatia Sunderland bao la pili.

Ilikuwa ni bahati mbaya sana kwa mchezaji Chamberlain, kijana wa miaka 18, katika siku ambayo ilielekea yeye alikuwa ameonyesha mchezo wa kuvutia sana katika mechi hiyo.

Kwa mara nyingine tena meneja Arsene Wenger anajipata akirushiwa lawama, hasa ikikumbukwa kwamba Jumatano iliyopita ilifungwa magoli 4-0 katika uwanja wa San Siro, Italia, ilipocheza na AC Milan katika mechi ya klabu bingwa barani Ulaya.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA