Rais wa Yanga SC, Eng. Hersi Said 🇹🇿, ameonyesha dhamira kubwa ya kuendelea kujifunza baada ya kuamua kurejea darasani kuongeza elimu zaidi kwa ajili ya kuimarisha uwezo wake wa kiuongozi na miradi anayoisimamia sasa pamoja na ile inayokuja.
Inaelezwa kuwa Eng. Hersi Said amejiunga na moja ya taasisi kubwa za elimu nchini Uingereza, inayojulikana kama University of Oxford, hatua inayotafsiriwa kama jitihada za kujiongezea maarifa kwa maendeleo makubwa zaidi ya baadaye.
Mashabiki wengi wa Yanga SC wamepokea hatua hiyo kwa furaha, wakiamini elimu hiyo itaongeza mchango mkubwa katika maendeleo ya klabu na miradi yake ya kimkakati. #KipengaSportUPDATES

Comments