CCM YATANGAZA RATIBA YA UCHAGUZI MDOGO WA ARUMERU MASHARIKI


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

Halmashauri Kuu ya CCM Taifa katika kikao chake cha siku moja chini ya
uenyekiti wa Mwenyekiti wa Taifa Dr. Jakaya M. Kikwete, pamoja na
mambo mengine imetoa ratiba ya mchakato wa kumpata mgombea wa CCM kwa
uchaguzi mdogo wa jimbo la Arumeru Mashariki.

Katika kikao chake hicho kilichofanyika tarehe 12/02/2012 mjini
Dodoma, NEC pia imetoa ratiba ya mchakato wa kuwapata wagombea udiwani
kwa tiketi ya CCM kwenye kata nane zilizotangazwa kufanya chaguzi
Ndogo na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

1. UBUNGE:
Katika nafasi ya Ubunge kwa Arumeru Mashariki, utaratibu utakaotumika
ni ule wa kupiga kura za maoni kwenye Mkutano Mkuu wa Jimbo.

(i) Tarehe 13 – 18/02/2012 Kuchukua na kurejesha fomu.
(ii) Tarehe 20/02/2012 Mkutano Mkuu wa Jimbo kupiga Kura za maoni.
(iii) Tarehe 21/02/2012 Kamati ya Siasa ya Wilaya kujadili Wagombea na kutoa
mapendekezo yake kwa Kamati ya Siasa ya Mkoa.
(iv) Tarehe 24/02/2012 Kamati ya Siasa ya Mkoa kujadili Kutoa
mapendekezo yake kwa Kamati kuu.

(v) Tarehe 27/02/2012 Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa kufanya
uteuzi wa mgombea wa Chama Cha Mapinduzi.
2. UDIWANI
Nafasi ya Udiwani katika kata 8 za Tanzania Bara Katika nafasi hii
kura za maoni zitapigwa kwenye Mikutano Mikuu ya Matawi.
(i) Tarehe 13 – 16/02/2012Kuchukua na kurejesha fomu.
(ii) Tarehe 17 – 21/02/2012 Kampeni za Uchaguzi kwenye Matawi.
(iii) Tarehe 22/02/2012Mikutano Mikuu ya Matawi kupiga kura za maoni.
(iv) Tarehe 25/02/2012 Kamati za Siasa za Wilaya kujadili wagombea na
kutoa mapendekezo yake kwa Kamati za Siasa za Mikoa.

(v) Tarehe 27/02/2012 Kamati za Siasa za Mikoa kujadili wagombea na
kutoa mapendekezo yake kwa Halmashauri Kuu za Mikoa.

(vi) Tarehe 29/02/2012 Halmashauri Kuu za Mikoa kufanya uteuzi wa wagombea.

Katika hatua nyingine Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imepokea maelezo
juu ya mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya na maelezo juu ya mgomo
wa madaktari nchini.

Kwa ujumla NEC imepokea maelezo hayo kutoka serikalini na kuiagiza
serikali kukamilisha mchakato wa kumaliza kabisa mgogoro wa madaktari
nchini na kuhakikisha migogoro ya namna hiyo inashughulikiwa mapema
ili isiwe na madhara makubwa kwa wananchi.

NEC imeridhishwa na jinsi mchakato wa upatikanaji wa Katiba mpya
unavyoendelea na kuipongeza serikali kwa jinsi inavyolisimamia swala
hilo. Imewataka wana CCM na wananchi wote kushiriki mchakato huo, huku
wakizingatia kutunza amani na utulivu uliopo nchini.

Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imewapongeza viongozi, wanachama na
wananchi wa Mkoa wa Mwanza kwa jinsi walivyofanikisha sherehe za miaka
35 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi ambapo kitaifa mwaka huu
zilifanyika mkoani humo.

Sherehe hizo ziliandaliwa na kufanikiwa kwa kiwango cha hali ya juu
kabisa, hivyo NEC inawapongeza kwa kufanikisha sherehe hizo.

Pamoja na Mkoa wa Mwanza NEC inawapongeza wanachama, viongozi na
wananchi kwa ujumla nchi nzima kwa jinsi walivyofanikisha sherehe hizo
za miaka 35 ya kuzaliwa kwa CCM kwenye maeneo yao.

Imetolewa na;
Nape Moses Nnauye
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.