HALI HII NI NDOTO KUPUNGUA KWA AJARI ZA BARABARANI MKOANI MBEYA, ASKARI USALAMA WA BARABARANI WAFUMBIA SUALA HILI?

Licha ya Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mbeya Advocate Nyombi, kuzuia magari ya mizigo maarufu kama Malori kubeba abiria, hali imekuwa tete kutokana na Askari wa usalama wa barabarani Kituo cha Mlowo, barabara ya Mlowo/Kamsamba wamekuwa wakiruhusu magari hayo kupakia abiria kupita kiasi kama inavyoonekana pichani. Mbali na askari hao kufanya ukaguzi hali hii imekuwa ikifanyika kila siku majira ya asubuhi na mchana.

Mtandao huu umeshuhudia gari hii ya mizigo ikiwa imebeba abiria na mizigo kama baiskeli, vinywaji ikiondoka kutoka Mlowo kuelekea Kamsamba wilaya ya Mbozi, licha ya kukaguliwa na Askari wa usalama wa barabarani na kuruhusiwa kuondoka, ambapo kwa hali hii inatishia usalama wa abiria. (Picha zote na Ezekiel Kamanga, Mbozi wa Mbeya Yetu Blog).

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

GSM ARIDHIA UJENZI WA UWANJA WA YANGA JANGWANI

WACHEZAJI YANGA WAGOMA KABISA KUFANYA MAZOEZI LEO, LWANDAMINA AIBUKA PEKE YAKE SHAMBA LA BIBI

DKT. MAJULE AMFANYIA MAPOKEZI MAKUBWA BALOZI WA CHINA NCHINI

HERSI KWENDA KUSOMA TENA CHUO KIKUU CHA OXFORD UINGEREZA

UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA MSALATO DODOMA KUANZA KUTUMIKA SEPTEMBA 2026

Wasifu wa Kizza Besigye

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA