JK AGAWA NG'OMBE LUKUKI LONGIDO

Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wakazi wa wilaya Longido muda mfupi baada ya kuwasili wilayani hapo ambapo aliongoza shughuli ya kutoa msaada wa ng’ombe zaidi ya elfu ishirini na tano na mbuzi zaidi ya elfu kumi na tano kwa wakazi wa wilaya za Longido,Ngorongoro na Monduli ambao mifugo yao yote iliangamia wakati wa kiangazi kikali.(photo by Freddy Maro)

Mmoja wa wazee wa Kimasai akimuombea dua Rais Jakaya Kikwete wilayani Longido Jumapili, wakati wa hafla ya uzinduzi wa wa mradi wa Serikali wa uwezeshaji mifugo (seed stock) kwa kaya za wafugaji waliopoteza mifugo yote kutokana na ukame msimu wa 2008-2009 na 2009-2010 iliyofanyika wilayani longido jumapili. (PICHA NA FRED MARO)
Mwanafunzi Godlisten Ole Olais anayesoma Kidato cha Pili katika Shule ya Sekondari ya Longido, akiteta jambo na Rais Jakaya Kikwete muda mfupi baada ya Rais kuwasili katika viwanja vya sekondari hiyo kuongoza uzinduzi wa wa mradi wa serikali wa uwezeshaji mifugo(seed stock) kwa kaya za wafugaji waliopoteza mifugo yote kutokana na ukame msimu wa 2008-2009 na 2009-2010 zilizofanyika wilayani longido jumapili.

Viongozi wa kabila la Kimasai (Laigwenani) wakimpa Rais Jakaya Kikwete zana za kijadi za uongozi mkuki na fimbo wakati wa hafla ya kukabidhi ng’ombe iliyofanyika wilayani Longido jumapili.

Mzee wa Kimasai mkazi wa Longido akimshukuru na kumuombea dua njema Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete baada ya mzee huyo kukabidhiwa ng’ombe watano na mbuzi watano wilayani Longido jana.Mzee huyo ni mmoja wa wafugaji waliopoteza mifugo yao yote kufuatia ukame mkali uliozikumba wilaya za Longido,Ngorongoro na Monduli
Baadhi ya vijana wakiwa juu ya mti kumuona na kumsikiliza Rais Jakaya Kikwete

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI