
Mchezaji wa timu ya Yanga Haruna Niyonzima akichuana na beki wa timu ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi kuu ya Vodacom uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jioni hii jijini Dar es salaam, Mpira umekwisha na Yanga imefanikiwa kuitandika Mtibwa Sugar Magoli 3-0 bila huruma katika kipindi cha pili cha mchezo huo.

Refarii wa mchezo huo akinyoosha mkono wake juu kuashiria timu ya Yanga ipige mpira wa adhabu kuelekea lango la timu ya Mtibwa Sugar.
Mmoja wa Mashabiki wa timu ya Yanga akiwa amejipaka masizi usoni mwake ikiwa ni moja ya staili ya ushangiliaji kwa timu yake.. (PICHA NA FULLSHANGWE BLOG)
Comments