LAKI MBILI WAJITOKEZA MPANGO WA "WEZESHWA NA SAFARI LAGER"

Meneja wa Bia ya Safari Lager ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Oscar Shelukindo (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo , kuhusu siku zilizosalia mpango wa kuwawezesha Wajasiriamali Wadogo Wadogo nchini uitwao "Wezeshwa na Safari Lager". Kushoto ni Meneja Uendeshaji wa Kampuni ya Intagrated Communicatins Limited inayoratibu mpango huo, Lawrence Andrew.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa makini kuchukua habari hiyo, Dar es Salaam.
Meneja Uendeshaji wa Kampuni ya Intagrated Communicatins Limited inayoratibu mpango huo, Lawrence Andrew (kushoto) akielezea zaidi kuhusu mpango huo
Shelukindo (kulia) akielezea mikakati mbalimbali ya kufanikisha mpango huo
Shelukindo akisisitiza jambo katika mkutano huo
Vyombo vya habari vikiwa kazini wakati Shelukindo akizungumza. (PICHA ZOTE NA KAMANDA MWAIKENDA)

SAFARI LAGER YATANGAZA KUSALIA MAJUMA MATATU YA MPANGO WA KUWAWEZESHA WAJASIRIAMALI WADOGOWADOGO NCHINI. “WEZESHWA NA SAFARI LAGER”
Dar es Salaam,Alhamisi February16, 2012: Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imetangaza maendeleo ya kampeni ya aina yake ya kuwatafuta na kuwawezesha wajasiriamali wadogowadogo katika shindano la wezeshwa na Safari Lager na unaweza kupata ruzuku ya kusaidia kuona njiaya mafanikio katika mikoa ya Mwanza,Mbeya na Arusha ambapo sasa zimesalia siku 21 kabla ya zoezi hilo kufungwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dasr es salaam,Menejawabiaya Safari Lager, Oscar Shelukindo alisema Bia ya safari Lager ilizindua program maalum ya kuwawezesha ya kufanikisha kuwawezesha wajasiriamali wadogowadogo nchini kupitia programu ya wezeshwa na Safari lager Novemba 24 jijini Dar Es Salaa ikiwa na lengo kuu la kuwasaidia wamiliki wa biashara ndogondogo naza kati kukuza biasharazao,

Alisema programu hiyo ilizinduliwa katika kanda kuu nne za Tbl ambazo ni kanda ya Dar Es Salaa,Kanda ya Ziwa,kanda Kaskazini na kanda ya nyanda za juu kusini ambapo wamiliki wa biashara ndogondogo walipaswa kuchukua fomu maalum toka katika bohari na viwanda vya Tbl katika mikoa yao au pia kuchukua fomu kwenye tovuti www.wezeshwa.co.tz au kutuma barua pepe kwenda info@wezeshwa.co.tz au unaweza kupiga simu nambari 0763 600041 (Dar es Salaam) 0763600042 (Arusha) 0763 600044 Mwanza) na 0763 600045 (Mbeya) namwishowakurudishafomuni 02Machi 2011
Alisema kwa hivi sasa programu hiyo inaelekea ukingoni ambapo hivi karibuni jopo la majaji walibobea katika elimu ya uendeshaji wa biashara wataanza mchakato wa kupitia fomu zote zilizotumwa ili kuweza kupata washindi kwa kila kanda.
Leo hii tunapenda kuwafahamisha watanzania kuwa zimebaki takribani majuma matatu kabla ya pazia la kuchukua na kuresha fomu kufungwa rasmi tarehe 02.03/2012 saa sita usiku hivyo napenda kuchukua nafasi hii kuwakumbusha wale wamiliki wa biashara ndondogo waliochukua fomu kurejesha katika vituo husika mapema na pia kwa wale ambao bado hawajachukua maamuzi ya kushiriki kufanya maamuzi hivi sasa maana muda umebakia mchache sana na kama tunavyofahamu sote Safari Lager imeandaa kiasi cha Shilingi milioni mia mbili ( 200,000,000) ambazo zitatolewa kwa wamiliki wa biashara kama ruzuku na pia wataalamu wetu watafanya mchakato wa kuwawezesha hao washindi ishirini kwa kila kanda kuweza kuwapatia semina na elimu ya ujasiriamali na namna ya kuendeleza na kukuza biashara zao,Alisema bwana Shelukindo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.