Mkuu wa Huduma za Tiba Jeshi la Wananchi Tanzania Meja Generali Adam Mwabulanga, akitowa maelezo ya mafanikio ya zoezi la kutoiwa huduma kwa Wananchi wenye matatizo ya Macho Zanzibar.
Meja Generali Devid Hogg, akizungumza na Mkuu wa Huduma za Tiba Jeshi, alipowasili katika Hospitali ya Bububu kuangalia maendeleo ya Zoezi la kuwafanyia uchunguzi wa Macho Wananchi mbalimbali waliofika hospitalinin hapo katika zoezi hilo.
Mkuu wa Hospitali ya Jeshi Bububu, akitowa Maelezo kwa Meja Generali wa Jeshi la Marekani ambae na Mkuu wa Utendaji wa Kivita na Mahusiano wa Afrika, David Hogg, katikati na kushoto Mkuu wa Huduma za Tiba Jeshi la Wananchi Tanzania Meja Generali Adam Mwabulanga, wakiwasili katika Hospitali ya Bububu kuangalia zoezi la kutowa huduma kwa Wananchi wenye matatizo ya Macho wa Zanzibar.
Mwananchi akifanyiwa kipimo kabla ya kufanyiwa upasuaji, katika zoezi hilo.linaloendelea katika Hospitali ya Bububu mpaka tarehe 17-2-2012
Wananchi wakifanyiwa uchunguzi wa kusoma herufi kwa kutumia miwani maalum,katika zoezi ya kufanyiwa uchunguzi wa macho kwa wananchi wa Zanzibar katika hospitali ya Bububu linalosimamiwa na Jeshi la Marekani kushirikiana na Madakatri wa Jeshi la Tanzania na Hospitali ya Mnazi Mmoja.
Madaktari Bingwa wa Jeshi la Marekani na Wazanzibar, wakiwafanyika Upasuaji baadhi ya Wananchi waliokutikana na matatizo ya macho katika zoezi hilo, linalosimamiwa na Madaktari wa Jeshi la Marekani.katika Hospitali ya Bububu.
Madaktari Bingwa wa Jeshi la Marekani wakimfanyia upasuaji mmoja wa Mwananchi aliefika kufanyiwa uchunguzi wa macho na kugundulikana ana matatizo na kufanyiwa upasuaji.kuondolewa mtoto wa jicho.
Kanali waJeshi la Marekani Dk. Carlton, akitowa maelezo jinsi ya mafanikio ya zoezi hilo kwa Wananchi wanaofika kupata huduma ya kufanyiwa uchunguzi wa macho.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.