MAMBO YA BUNGENI LEO


.Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda akiingia ndani ya ukumbi wa bunge leo mjini kuongoza kikao cha tisa cha mkutano wa sita wabunge ambapo bunge linahitimisha shughuli zake mjini Dodoma. Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
Mbunge wa Same Mashariki Anna Kilango akijadili jambo na Mwanasheria mkuu wa serikali Jaji Frederick Werema ndani ya ukumbi wa Bunge leo wakati wa kipindi cha maswali na majibu mjini Dodoma.
Mbunge wa Singida mjini Mohammed Dewji akimsikiliza kwa makini Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Uhusiano na Uratibu Stephen Wasira ndani ya ukumbi wa bunge leo mjini Dodoma.
Wajumbe na Viongozi wa chama cha wamiliki wa shule Vyuo na shule binafsi (TAMONGSCO) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutoka ndani ya ukumbi wa bunge leo mjini Dodoma. Viongozi hao wapo bungeni Dodoma kukutana na kamati ya kudumu ya bunge ya huduma za jamii kwa lengo la kuhimiza ushirikiano kati yao na wabunge pamoja na serikali ili kubadilishana uzoefu na kujadili changamoto zinazoikabili sekta binafsi ya elimu nchini Tanzania.
Mbunge wa Bumbuli January Makamba akiwasilisha Hoja binafsi kuhusu sheria ya udhibiti wa shughuli za upangaji nyumba za makazi aliyoitoa chini ya kanuni ya 54 (1) ya kanuni za bunge toleo la 2007 ya kuliomba bunge kuazimia kwa kauli moja ,kuitaka serikali katika mkutano ujao wa saba kuleta Muswaada wa Sheria ya kudhibiti Upangaji wa Nyumba na Makazi kufuatia malalamiko mengi kutoka kwa wananchi wanaoishi mijini kutokana na adha wanazopata katika kutafuta nyumba za kupanga au kuishi kwenye nyumba hizo.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda akiwasalimia viongozi na wachezaji wa timu ya Villa Squard ya Kinondoni jijini Dar es salaam waliofika bungeni hapo kuona shughuli mbalimbali zinazofanywa na bunge.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda akifurahia jambo na wanafunzi wa shule ya sekondari Hijra ya mjini Dodoma nje ya ukumbi wa Bunge Dodom

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.