MASHINDANO YA SAFARI LAGER NYAMA CHOMA KUANZA MBEYA,DAR

Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo (katikati) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, kuhusu maandalizi ya mashindano ya Safari Lager Nyama choma katika mikoa ya Mbeya na Dar es Salaam. Wengine ni majaji wa mashindano hayo.
Jaji Mkuu wa mashindano ya Safari Lager Nyama Choma, Douglas Sakibu (kushoto), akionesha katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, vifaa maalum vitakavyotumika kupima ubora wa nyama katika mashindano hayo. Kulia ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo. (PICHA NA KAMANDA MWAIKENDA)

MASHINDANO YA KUCHOMA NYAMA
“SAFARI LAGER NYAMA CHOMA 2012” YATANGAZA BAA ZILIZOCHAGULIWA DAR ES SALAAM NA MBEYA.

Dar es Salaam, Jumanne Feb 21, 2012: Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imetangaza majina ya baa bora zilizochaguliwa kuingia kwenye mchujo wa awali kwa mikoa ya Dar es salaam na Mbeya kwenye yale mashindano ya aina yake na ya kuvutia ya kuchoma nyama yajulikanayo kama “Safari Lager Nyama Choma 2012”

Mashindano haya hushirikisha majiko ya baa hizo zilizochaguliwa mikoa husika ambapo utaratibu wa kuzipata ulikuwa ni kwa walaji wa nyama choma na wanywaji wa bia ya Safari kuchagua baa na jiko ambalo wanaamini kuwa linachoma nyama bomba zaidi kuliko zote.

Akizitaja baa hizo kwenye mkutano na waandishi wa habari jiji Dar es salaam meneja wa Bia ya Safari Lager Bw. Oscar Shelukindo alisema zoezi la kupata baar za mikoa ya Dar Es Salaam na Mbeya limekamilika ambapo kwa mkoa wa Dar Es Salaam baa zilizochaguliwa ni ishirini ambazo niHuduma Bar,Rosehill garden,Kilwa Road Pub,Pentagon Pub,Texedo Garden,Gadafi Square,Angels Pub,Fyatanga Bar,Jambo Lee,Hongera Bar,Braek Point Bar,Meeda Bar,Titanic Bar,Mangi Bar,Africenter Bar,Kisuma bar na Twiga bar wakati Mkoa wa Mbeya zimechagu ni Mbeya Carnival,City Pub,2000 Grocery,Kalembo Bar,Shaba Bar,Makasini Bar,Freepark Bar,Savoy Bar,Double J Bar na Coasini Bar. Ambapo alisema baa hizi zimepatikana baada ya wakazi wa mikoa yote miwili kutafakari na hatimae kuamua kuzipigia kura baa hizo kulingana na umahiri wao katika uandaaji na uchomaji wa nyama choma.

Kwa sasa hatua inayofuata ni jopo la majaji kuanza kutembelea hizo bar na majiko hayo na hatimae kupata washindi watano bora kwa kila mkoa ambao ndio watapata nafasi ya kupambana katika tamasha kubwa la wazi litakalofanyika katika kila mkoa na hatimae kupatikana kwa mabingwa wa kila mkoa.

Kwa upande wake Jaji Mkuu wa Mashindano hayo Jaji Douglas Sakibu aliwataka wale wamiliki na wachoma nyama wote waliofanikiwa kuingia katika hatua hii muhimu kujianda vyema ambapo zoezi la kutembelea baa hizo litaanzia jijini Mbea ambapo Jumatano ya Feb24,2012 washindi wa mkoa wa Mbeya watapata nafasi ya kushiriki kwenye semina maalumu itakayoendeshwa na majaji hao ambao ni wataalamu waliobobea katika Nyanja hizo wakiwa wote wamepata mafunzo toka katika nchi mbalimbali zilizopiga hatua kwenye uandaaji wa nyama choma.

Alisema miongoni mwa mafunzo yatakayotolewa ni pamoja na namna ya kuchagua ,kuandaa na kuchoma nyama ,kiasi cha ubaridi unaopaswa kuwa kwenye nyama na usafi wa mazingira”Kwa kweli hii ni fursa nzuri kwa wale wote waliochaguliwa kuweza kupata nafasi ya kujifunza mambo mengi hii elimu ilipaswa kulipiwa lakini kupitia bia ya Safari tutatoa bure kabisa lakini pia tutatoa vyeti kwa wachoma nyama na baa zote zilizofanikiwa katika hatua hii muhimu”alisema Douglas.
Mashindano ya mwaka huu yatafanyika katika mikoa mitano ambayo ni; Dar Es Salaam, Kilimanjaro, Arusha,Mbeya.na Mwanza.na Mwanza
Akitaja zawadi za washindi, Shelukindo alisema; baa itakayoshika nafasi ya kwanza itajinyakulia shilingi Milioni Moja, mshindi wa pili, Laki Nane, Mshindi wa Tatu laki Sita, Nafasi ya Nne; Laki Nne na nafasi ya Tano shilingi Laki Mbili. Zawadi hizi zimegawanywa kwa kila mkoa.

Utaratibu wa kupata baa zitakazoshiriki mashindano haya utaendeshwa kwa njia ya simu, ambapo wananchi watatakiwa kutuma ujumbe mfupi usemao “Safari kisha Mkoa uliopo ikifuatiwa na jina la Baa” kisha tuma kwenda namba 0763 514 514 Utapokea ujumbe kukuhakikishia kuwa kura yako imepokelewa na kwa sasa wakazi wa mikoa ya Kilimanjaro,Arusha na Mwanza bado wanayonafasi sasa ya kuendelea kupiga kura na kuchagua baa na jiko ambalo wanaamini kuwa linaandaa na kuchoma nyama bombo zaidi katika mkoa wao
.Alisema hii ni fursa ya pekee kwa wachoma nyama na wenye mabaa kuweza kupata mafunzo yakinifu juu ya uandaaji na uchomaji wa nyama toka kwa wataalam wenye ujuzi na waliobobea kwenye taaluma hiyo ili kuweza kukuza na kuboresha biashara zao na hatimae kufikisha kwa wateja kitu kilichokuwa na ubora wa hali ya juu.

Mashindano ya Safari Nyama Choma mwaka huu yanafanyika kwa mara ya nne ambapo mwaka jana washindi wa Jiji la Dar Es Salaam walikuwa Kisuma Bar ya Temeke Mwembe Yanga,Mbeya walikuwa Mbeya Canival,Kilimanjaro walikuwa Makanyaga bar ya Soweto na Arusha walikuwa SongaMbele Bar ya Sakina.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.