MKAZI WA UYOLE APELEKWA MAHAKAMANI KWA KOSA LA KUKUTWA NA KETE 26 ZA BANGI - MBEYA






Pichani ni Kete za madawa ya kulevya.
*******
Habari na Mwandishi wetu.
Mapinduzi Magalasi mwenye umri wa miaka 34 mkazi wa Uyole jijini Mbeya amefikishwa katika mahakama ya mkoa kwa kosa la kukutwa na bangi kete ishirini na sita.

Akisoma shitaka hilo mbele ya hakim mkazi Francis Kishenyi mwanasheria wa serikali Achilesi Mlisa amesema Agosti 22 2011 maeneo ya Uyole mshitakiwa alikutwa na kete 26 za bangi kinyume na kifungu cha sheria namba 12 (d) sura 95 marekebisho ya mwaka 2002.

Hata hivyo mshitakiwa amekana shitaka hilo na amerudishwa rumande kwa kukosa mdhamini mwenye fedha shilingi laki mbili na barua kutoka kwa mtendaji na kesi hiyo itatajwa tena Februari 21 mwaka huu.CHANZO; MBEYA YETU BLOG

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

GSM ARIDHIA UJENZI WA UWANJA WA YANGA JANGWANI

WACHEZAJI YANGA WAGOMA KABISA KUFANYA MAZOEZI LEO, LWANDAMINA AIBUKA PEKE YAKE SHAMBA LA BIBI

DKT. MAJULE AMFANYIA MAPOKEZI MAKUBWA BALOZI WA CHINA NCHINI

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA

HERSI KWENDA KUSOMA TENA CHUO KIKUU CHA OXFORD UINGEREZA

Wasifu wa Kizza Besigye

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda