Mbunifu wa mavazi mama Asia Idarous Khamsin wa Fabak Fashion ambaye pia ni muandaaji wa onesho la Lady and Red 'Reloaded ' 2012 akiwa katika mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia onesho linalotarajiwa kufanyika Februari 10, 2011 katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Kulia ni Maulidi Mlawa ambaye ni Katibu wa Kikundi cha Kikale Youth Care kilichipo wilayani Rufiji. Onesho hilo linatarajiwa kuwakutanisha wabunifu wapatao 30 ambao wataonyesha mavazi yao.
Meneja wa kinywaji cha Redds Original Victoria Kimaro ambao ni wadhamini wakuu wa onesho hilo.
Mbunifu wa mavazi mama Asia Idarous Khamsin (wa pili kulia) wa Fabak Fashion ambaye pia ni muandaaji wa onesho la Lady and Red 'Reloaded ' 2012 akiwa katika mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia onyesho linalotarajiwa kufanyika Februari 10, 2011 katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Kulia ni Bw. Maulidi Mlawa ambaye ni Katibu wa Kikundi cha Kikale Youth Care kilichipo wilayani Rufiji na Meneja wa kinywaji cha Redds Original, Victoria Kimaro ambao ni wadhamini wakuu wa onesho hilo. Onyesho hilo linatarajiwa kuwakutanisha wabunifu wapatao 30 ambao wataonesha mavazi yao.
Katibu wa Kikundi cha Kikale Youth Care kilichipo wilayani Rufiji Bw. Mauldi Mlawa akifafanua jambo kuhusu kituo maalum cha kusaidia waathirka wa dawa za kulevya kiitwacho "Kikale Youth Care Group" kinachotarajiwa kufunguliwa Rufiji ambapo Mbunifu wa mavazi mama Asia Idarous Khamsin wa Fabak Fashion ambaye pia ni muandaaji wa onyesho la Lady and Red 'Reloaded ' 2012 atachangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa kituo. Kushoto ni Meneja wa kinywaji cha Redds Original Victoria Kimaro ambao ni wadhamini wakuu wa onesho hilo. Picha na Habari na Mdau C.A. Kajuna.
--
Onyesho la mavazi lijulikanalo kwa jina la 'Lady in Red 2012' linaloandaliwa na mama wa mitindo Tanzania Asia Isarous Khamsin ni la saba kwa mwaka huu.


Mama Asia Idarous Khamsin atakuwa anatimiza maonesho ya mavazi yapatayo 100 kwa Tanzania tu mbali na maonesho mengine ambayo amefanya nchi za nje,Kwa hivi sasa Asia Idarous Khamsin anafanya kazi zake Tanzania na USA.


Mwaka huu onyesho hilo litazindua kituo maalum cha kusaidia waathirka wa dawa za kulenywa kiitwacho "Kikale Youth Care Group"
Wabunifu wapatao 30 watapanda jukwaani siku hiyo kuonyesha miotindo tofauti ya mavazi na tiketi zimeanza kuuzwa FABAK Fashions, Mikocheni Dar es Salaam na kwa mawasiliano zaidi unaweza kupiga 0784263363.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*