Rais Jakaya Kikwete wa nne kutoka (kulia) akishiriki katika matembezi ya kuchangia shilingi Bilioni moja kwa ajili ya ujenzi wa jengo la akina mama wenye matatizo ya ugonjwa wa Fistula katika hospitali ya CCBRT leo asubuhi jijini Dar es salaam, matembezi hayo yameanzia katika hoteli ya Golden Tulip na kumalizika katika Hospitali ya CCBRT Mikocheni, matembezi hayo yameandaliwa kwa pamoja na kampuni ya Vodacom Tanzania, Vodafone pamoja na hospitali ya CCBRT Kampeni hiyo inajulikana kama (Finde your Moyo).
Rais Jakaya Kikwete, Katibu Mkuu wa Chadema, Willbroad Slaa na Mkurugenzi wa Huduma za Jamii wa CCBRT, Brenda Msangi wakishiriki katika mazoezi alipokuwa katika matembezi hayo leo.
Rene Meza Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania akitoa hotuba yake kabla ya kuanza kwa matembezi hayo leo asubuhi. Watu mbalimbali waliojitokeza katika matembezi hayo wakiwa katika hoteli ya Golden Tulip leo asubuhi.
Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya CCBRT Bw. Wilbroad Slaa akizungumza na Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba.
Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba akizungumza na Rene Meza Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania.
Wakiwa katika mzungumzo kabla ya kuanza kwa matembezi hayo kulia ni Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es salaam ya kipolizi Suleiman Kova, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Jordan Rugimbana na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hadji Mponda.
Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu Salva Rweyemamu akijadili jambo na Meneja Udhamini na Matukio wa Vodacom Tanzania Rukia Mtingwa. Watu mbalimbali walioshiriki katika matembezi hayo
Kulia ni Grace Lyon wa Vodacom Tanzania, Meneja wa Vodacom Foundation Yesaya Mwakifulefule na Matina Nkurlu Meneja wa kitengo cha habari za Mtandao Vodacom Tanzania.
Wadau wangu wakubwa kulia ni Bw. Philip Seyayi aka (Shvangirai) kutoka JWT na Ofisa Udhamini wa Vodacom Tanzania Ibrahim Kaude wakipata viroba vyao! Ah ni utani tu jamani hii ni Juice.

Mazoezi yanaendelea.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

WAZIRI BASHE APIGA MARUFUKU WASIOSOMEA KILIMO KUUZA PEMBEJEO

CHAMA KIPYA CHA WALIMU WAMUOMBA RAIS SAMIA AINGILE KATI MAKATO YA WANACHAMA WAO

NILIYOYABAINI KATIKA TRENI YA SGR DAR ,MORO HADI DODOMA … KADOGOSA REKEBISHENI MAMBO HAYA MTANIKUMBUKA

DK. KIKWETE AZINDUA KITUO CHA AFYA KIZIMKAZI, APONGEZA MAENDELEO ZANZIBAR

KOCHA WA MAMELODI ASIMAMISHWA KWA KUWAPIGA CHABO WACHEZAJI WAKE WA KIKE