SHINDA VITA JUU YA WIVU.......UKIMBIE WIVU....JUA JINSI YA KU MANAGE WIVU...



HIZI HAPA NJIA KADHAA ZA KUWEZA KUSHINDANA NA WIVU:

Kuna watu inatokea wanakuwa na bahati ya kuwa na vitu vyote tu
Mume tajiri, kazi nzuri, mshahara mnono na nafasi zingine za juu katika maisha.
Ni rahisi kuwa envy na kuwaonea wivu.
Lakini ukiutumia wivu huo kwa njia nzuri unaweza kuwa wa manufaa
Na ukiutumia wivu vibaya unaweza ukaumiza zaidi hisia zako mwenyewe.

Inawezekana kabisa kuwaangalia watu waliofanikiwa na kufurahia mafanikio yao Lakini wivu unaanza kukula pale unapotamani kuwa kama wao
Inasemekana wivu unawaathiri sana watu wenye umri chini ya miaka 45
Lakini ukiangalia kwa undani watu wengi waliofanikiwa, wamepitia njia nyingi sana hadi kufikia hapo walipo.


Je! uko tayari kupitia magumu kama yao? Au unaona wivu tu?

Watu wengine wamesota zaidi ya miaka 20 kufikia mafanikio
Sacrifices, kutokulala usiku na mafanikio mengine sio hata katika njia halali
Wakati watu wengi wenye wivu wanahitaji mafanikio ya haraka haraka na njia za mkato
bila kujua kuwa ili ufanikiwe ni lazima utumike kisawa sawa
Zaidi ya hapo labda ucheze lotto/Bingo ndio njia pekee na rahisi lakini pia mpk uwe na bahati


Wivu unachangia mtu kuwa na roho mbaya (chuki) na kutojiamini

Na wivu unamuumiza zaidi mtu anaeona wivu, kuliko yule anaeonewa wivu

Kama hufurahii vile ulivyo, au kile ulicho nacho

Wekeza nguvu katika kupanga mipango ya baadae ya kuboresha maisha zaidi kuliko kujijazia chuki na kupoteza muda kufikiria kitu ambacho huwezi kuwa nacho.
Ni ngumu lakini ukiipa muda na kujitolea utaweza
SHINDA VITA DHIDI YA WIVU

1. Kuliko kupoteza muda kwa kile ambacho huna, weka nia katika kuendeleza kidogo chochote ulicho nacho, Ndoto zako, kipaji chako hivyo ndio vyanzo vya mafanikio yako


2. Ni vizuri kuwa mshindani, kwa njia ilio sahihi kwakuwa tupo kwenye dunia ya ushindani.
Lakini uwe na tahadhari na ujiepushe na hatari ya kushindana ili uwe bora kuliko wengine

Jikubali kwanza na ujitambue wewe kama ulivyo, nini malengo/makusudio yako katika maisha.
Ukubali wazi kuwa itachukua muda na sio kazi rahisi kufikia walipofikia wengine bila kufanya kazi kwa bidii


3.Ukishaamua nini cha muhimu kwako, elekea katika kutafuta kazi zenye manufaa
. Kubali kujifunza kadri uwezavyo kutoka kwa wakubwa, au waliokutangulia kiujuzi ili kuongeza ujuzi wa zaidi ya kile unachokifahamu, huku ukikubali kukosolewa

Ndio hapo na wewe unaweza kumiliki simu 2 moja ikiwemo Back Berry kama unahitaji. Lakini jitahidi ununue kile kitu ambacho tu ndio uwezo wako
Na sio kuwa na kitu ili mradi watu wakuone kuwa umefanikiwa kukipata hata kama haukihitaji au hakiko ndani ya uwezo wako

4. Kubali na ridhika na ulicho nacho hata kama ni kidogo, jua jinsi ya kupanga na kukitumia kikakidhi mahitaji yako

5. Tafuta watu waliofanikiwa uongee nao, wauliza njia na jinsi gani wamefanya mpaka kufikia mafanikio walio nayo (Japo wengine huwa hawasemi ukweli) ila sikiliza halafu chuja

6. Kama una mwili mkubwa na unahitaji kupungua, ni lazima ufanye mazoezi na ufatishe njia unazoelekezwa ili kupata mwili unaouutaka
Sio kwa kukaa nyumbani unaendelea kula na kumchukia mtu mwembamba kwa kumtoa kasoro
Kama unahitaji kuanzisha biashara nenda kwenye seminars zinazohusu mambo ya biashara ukajifunze ili ujue wapi pa kuanzia
Chochote unachotaka kufanikiwa nacho ni lazima ukitumikieJINSI YA KUKABILIANA NA WIVU

1. Jiangalie na ukubali kuwa una wivu, halafu itumie hiyo nafasi kama silaha ya kukujenga. Ni ngumu sana watu kukubali kuwa wana wivu, na hilo ni tatizo

2. Ni rahisi kukutwa katika hali ya kuamini kuwa watu matajiri ndio washindi na maskini ni loosers lakini sio kweli.

Usiangalie mtu kutokana na kiasi gani alicho nacho, angalia vitu ambavyo ni vya muhimu

Kama utu, ukarimu, ukweli na usimtathmini mtu kutokana na mfuko wake.
Unaweza kuangalia mambo yanayotamanisha kwa nje kama hujui ki undani yakakufanya ujisikie mnyonge na kuyadharau maisha yako binafsi

3. Kama ukimuonesha roho mbaya mtu unaetamani maisha kama yake haitasaidia, inaweza kuwa mbaya zaidi maana hata kama ilikuwa akupe msaada hutapata kitu
Kama umefanya hivyo rudi ukaombe msamaha

4. Kama huwezi kuondokana na hali ya wivu, iongelee na uelezee hisia zako kwa mtu wako yoyote wa karibu itasaidia

Wivu unaweza kukupelekea katika matatizo ya kuwa na stress zisizo isha, blood presure na kutokulala usiku unakesha ukiwaza


KILA KHERI KATIKA KUJARIBU KUJIKOMBOA NA GONJWA LA WIVU

NI UGONJWA AMBAO UNAKUATHIRI ZAIDI WEWE ULIE NAO KULIKO HATA YULE AMBAE UNAMUONEA WIVU. Chanzo Lady Jay Dee Blog

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI