SIMBA, AZAM NGOMA NZITO LEO

Kikosi cha Simba
Azam FC wakipasha moto mwili

BAADA ya mashabiki wa soka nchini kushiba maneno ya majigambo toka kwa makocha wa timu za Simba na Azam FC kuelekea pambano lao Ligi Kuu Bara, sasa ni zamu ya kushuhudia vitendo wakati vikosi vyao zitakaposhuka kwenye Uwanja wa Taifa kusaka pointi tatu muhimu leo hii.

Makocha hao, Milovan Cirkovic wa Simba na Stewart Hall wa Azam, kwa wiki nzima sasa hawakukaukiwa maneno vinywani kabla ya pambano hilo linalotarajia kuwa kiini cha burudani ya wiki kwa mashabiki wa Ligi Kuu Bara.
Simba inashuka dimbani ikiwa na kumbukumbu ya vipigo viwili, kwanza kile cha mabao 2-0 mwezi mmoja uliopita toka Azam wakati wa michuano ya Kombe la Mapinduzi, na kisha kipigo cha bao 1-0 katika mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Villa Squad.

Kwa maana hiyo, Simba itashuka dimbani kwanza kulipa kisasi cha kufungwa na Azam, na pia kutibu 'majeraha' ya kipigo toka Villa kilichowakera zaidi mashabiki wake.

Ushindi au sare dhidi ya Azam utairejeshe Simba kileleni mwa msimamo baada ya kushushwa katikati ya wiki hii kwa tofauti ya mabao ya kufunga na mahasimu wao Yanga.

Nayo Azam iliyotangaza kuwania taji la ubingwa simu huu kwa udi na uvumba, itaongeza msisimko wa kipute hicho kwa kusaka pointi tatu ambazo ikiwa itafanikiwa itakuwa imefikisha pointi 35 kutoka 32 za sasa na kuongoza msimamo.

Furaha kubwa kwa mashabiki wa Simba ni kurejea uwanjani mshambuliaji wao Felix Sunzu aliyekuwa majeruhi, huku Azam nao wakisherehekea kurejea uwanjani kwa kiungo wao mahiri Kipre Bolou aliyekwamishwa hati ya uhamisho ya kimataifa(ITC).

Leo hii pia mbali na mechi ya Simba na Azam, kutakuwa na patashika nyingine kati Toto African itakayowasubiri Moro United kwenye uwanja wa CCM Kirumba, huku Villa Squad itakuwa mgeni wa Polisi Dodoma kwenye dimba la Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Moto wa ligi hiyo unaogusa mzunguko wa 17 sasa, utakuwa pia kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga wakati wenyeji Coastal Union watakapopepetana na African Lyon, kama ilivyo kwa timu za maafande za JKT Oljoro na JKT Ruvu zitakazokuwa zinaumana kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.

Katika hatua nyingine, Shirikisho la Soka Tanzania(TFF), limesema mchezo baina ya Kagera Sugar na Mtibwa Sugar uliokuwa ufanyike kesho, sasa utachezwa Jumatatu.

Afisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alisema jana kuwa mabadiliko hayo yamekuja kufuatia Uwanja wa Kaitaba wa mjini Bukoba ambao mechi hiyo imepangwa kufanyika kutolewa kwa shughuli nyingine za kijamii.


Aliongeza kuwa mabadiliko hayo pia yanaihusu mechi kati ya Toto Africans na Mtibwa Sugar iliyokuwa ichezwe Februari 15 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba ambayo sasa itachezwa Februari 16.

Chanzo;Gazeti la Mwananchi

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.