SUARES AKATAA KUMPA MKONO EVRA

Luis Suarez kukataa kumpa mkono Patrice Evra kabla ya mechi kati ya Manchester United na Liverpool ndio jambo ambalo mashabiki wengi watalikumbuka katika mechi iliyochezwa Jumamosi uwanja wa Old Trafford, na ambayo wenyeji walipata ushindi wa magoli 2-1.

Suarez na Evra walikutana kwa mara ya kwanza katika mechi hiyo ya ligi ya Premier, mara ya mwisho wakiwa uwanjani Anfield mwezi Oktoba, katika mechi ambayo mchezaji Suarez, kutoka Uruguay, alitamka maneno ya ubaguzi wa rangi dhidi ya mchezaji wa ulinzi Evra, na ambayo yalisababisha kupewa adhabu ya kutocheza katika mechi nane.

Katika shughuli za kiutaratibu za wachezaji kupeana mkono, Suarez aliupuuza mkono wa Evra.

Evra alijitahidi kumsogezea mkono wake, lakini kabisa Suarez alikataa kabisa kuunyosha mkono wake.

Kutokana na hayo, mlinzi Rio Ferdinand naye alikataa kumpa mkono mshambulizi huyo wa Liverpool.

Lakini licha ya Suarez kuelekea kuonyesha utovu wa nidhamu, uwanjani Wayne Rooney aliweza kuifungia Manchester United magoli mawili katika muda wa dakika nne, kipindi cha pili.

Suarez alikuwa anaonekana wazi anakerwa na kukosa kupata bao, lakini Liverpool walipata nafasi ya kuondoka na bao moja, wakati Michael Carrick alipoadhibiwa kwa kucheza vibaya, na kufuatia mkwaju wa Charlie Adam kudunda baada ya kumgonga Ferdinand, Suarez alifunga bao.

Mchango wa Rooney katika mechi hiyo sasa umeiwezesha Manchester United kuwa kileleni katika ligi kuu ya Premier, huku jirani Manchester City ikisubiri kucheza na Aston Villa siku ya Jumamosi, na pengine kuweza tena kuendelea kuongoza ligi.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA