SUAREZ AOMBA RADHI

Mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez na meneja wake Kenny Dalglish wameomba radhi kufuatia Suarez kukataa kumpa mkono Patrice Evra kabla ya mechi siku ya Jumamosi.

"Nimezungumza na meneja baada ya mchezo wa Old Trafford na nimetambua kuwa nilikosea," amesema Suarez katika taarifa iliyotolewa na klabu hiyo.

"Kila mmoja wetu ana jukumu la kuiwakilisha klabu hii katika mtindo unaofaa," alisema siku ya Jumapili.

"Jukumu hilo pia ninalo mimi kama meneja wa Liverpool.

"Nilipozungumza kwenye TV baada ya mchezo sikuwa nafahamu kilichotokea, lakini pia siku fanya kile kinachotarajiwa kufanywa na meneja wa Liverpool katika mahojiano, na ningependa kuomba radhi kwa hilo."

Manchester United ilitoa taarifa ikisema: "Manchester United inawashukuru Liverpool kwa kuomba radhi kufuatia matukio ya siku ya Jumamosi. Kila mmoja Old Trafford anataka kuondokana na jambo hilo.

"Historia ya vilabu vyetu viwili ni ya mafanikio na uhasama katika soka la Uingereza. Hilo ndio liwe lengo letu siku za usoni kwa mashabiki wanaozipenda timu hizi."

Suarez alifungiwa kucheza mechi nane kwa kumbagua na kumtusi Evra wakati wa mchezo wa ligi mwezi Oktoba mwaka jana.

Kukataa kwake kumpa mkono Evra siku ya Jumamosi kulichangia kuufanya mchezo huo kuwa wa vuta nikuvute ambapo United walishinda 2-1.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI