TAARIFA LUKUKI KUTOKA TFF

VILLA SQUAD, SIMBA ZAINGIZA MIL 30/-
Mechi namba 107 ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Villa Squad na Simba iliyochezwa Februari 4 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 30,017,000.
Watazamaji waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo ni 8,698 ambapo kiingilio kilikuwa sh. 3,000 kwa viti vya bluu na kijani, sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 10,000 kwa VIP C na B na sh. 15,000 VIP A.
Baada ya kuondoa asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni sh. 4,578,864.41 fedha zilizobaki zilikuwa sh. 25,438,135.59. Gharama za awali za mechi zilikuwa nauli ya ndani kwa waamuzi sh. 10,000, nauli ya ndani kwa kamishna wa mchezo sh. 10,000.
Posho ya kujikimu kwa mwamuzi wa akiba sh. 30,000, gharama za tiketi sh. 3,960,000, umeme sh. 300,000, usafi na ulinzi kwa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina (Beijing Construction) sh. 2,000,000. Nyingine ni Jichangie ambayo ni sh. 200 kwa kila tiketi; kila klabu ilipata sh. 608,860 wakati Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) kilipata sh. 521,880.
Mgawo baada ya gharama za awali; uwanja na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kila moja ilipata sh. 1,503,853.56, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 751,926.78, gharama za mechi sh. 1,503,853.56, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 150,385.36, DRFA sh. 601,541.42 na kila klabu ilipata sh. 4,511,560.68.
MUJUNI KUPIGA KIPENGA RWANDA
Mwamuzi Israel Mujuni wa Tanzania ameteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kuchezesha mechi ya marudiano ya raundi ya mchujo ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya APR ya Rwanda na Tusker ya Kenya itakayochezwa jijini Kigali kati ya Machi 2, 3 na 4 mwaka huu.
Mujuni atasaidiwa na Samuel Mpenzu na Khamis Maswa kutoka Tanzania wakati mwamuzi wa akiba katika mechi hiyo namba 18 atakuwa Louis Hakizimana wa Rwanda.
Kamishna wa mchezo huo atakuwa Aboubacar Nkejimana kutoka Burundi.
Nayo Mafunzo ya Zanzibar katika mechi yake ya kwanza katika raundi ya mchujo ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Muculmana de Maputo ya Msumbiji itakayofanyika mjini Zanzibar kati ya Februari 17, 18 na 19 mwaka huu itachezeshwa na waamuzi kutoka Shelisheli.
Bernard Camille ndiye atakayekuwa mwamuzi wa kati huku akisaidiwa na Steve Marie na Gilbert Lista. Mwamuzi wa akiba katika mechi hiyo namba 27 atakuwa Ramadhan Ibada wa Tanzania wakati Kamishna atakuwa Ali Waiswa kutoka Uganda.
Kwa mujibu wa CAF, timu 13 bora zenyewe zimeingia moja katika raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Timu hizo ni Coton Sport (Cameroon), El Ahly (Misri), Djoliba (Mali), Stade Malien (Mali), MAS (Morocco), Raja (Morocco), Sunshine Stars (Nigeria), TP Mazembe (Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), El Hilal (Sudan), El Merrikh (Sudan), EST (Tunisia), ESS (Tunisia) na Dynamos (Zimbabwe).
VIINGILIO UWANJA WA CHAMAZI- AZAM
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limefanyia marekebisho viingilio vya mechi za Ligi Kuu ya Vodacom zitakazochezwa katika Uwanja wa Azam ulioko eneo la Chamazi, Dar es Salaam.
Viingilio katika mechi za uwanja huo sasa vitakuwa sh. 1,000 kwa mzunguko na sh. 5,000 kwa jukwaa kuu badala ya vile vya awali vya sh. 3,000 kwa mzunguko na sh. 10,000 kwa jukwaa kuu. Mabadiliko hayo yalianza kwenye mechi ya jana kati ya Azam na JKT Oljoro.
Hata hivyo, viingilio hivyo havitatumika kwa mechi zitakazohusu mechi ambazo timu za Simba na Yanga zitacheza kwenye uwanja huo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI