Tamasha la Pasaka Mwanza lahamishiwa Dodoma

Na Mwandishi Wetu

TAMASHA la Pasaka lililopangwa kufanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, limehamishwa na sasa litafanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Awali, tamasha hilo lilipangwa kufanyika Mwanza Jumatatu ya Pasaka, Aprili 9 mwaka huu, lakini sasa onesho hilo litafanyika Dodoma siku hiyo.

Kwa mujibu wa Msama ambaye ni Mkurugenzi wa Msama Promotions, mabadiliko hayo yamefanyika kutokana na maombi ya wadau mbalimbali.

Hayo ni mabadiliko ya mara ya kwanza kufanywa na Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo chini ya Mwenyekiti wake, Alex Msama, aliyesema wangezingatia na kuheshimu maombi ya wanafunzi wa vyuo vikuu vilivyopo Dodoma wakiwamo wa Udom na wakazi wengine.

Onesho la kwanza la tamasha la Pasaka linatarajiwa kurindima Sikukuu ya Pasaka Aprili 8 mwaka huu kwenye ukumbi utakaotangazwa baadaye, Dar es Salaam.

Msama alisema Dar es Salaam jana kuwa tamasha la Pasaka litapambwa na waimbaji nguli wa nyimbo za kumsifu Mungu wakiwamo wa hapa nchini na kutoka nje ya nchi kama Kenya, Zambia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Afrika Kusini, Uganda na Rwanda ambao wafanyiwa taratibu za kupata vibali.

Tamasha la Pasaka la mwaka huu lina malengo ya kuchangisha fedha kwa ajili ya watoto yatima, kuwasaidia mitaji ya biashara wajane wasiojiweza.

Msama alisisitiza kuwa kwa vile ni tamasha la kimataifa, wafanyabiasha hawana budi kujitokeza kudhamini, na akabainisha milango iko wazi.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU