TBL YADHAMINI BONANZA LA WANAHABARI KWA MILIONI 60

Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, kuhusu udhamini wa Tamasha la Vyombo vya Habari likalofanyika Machi 24, mwaka huu. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Waadishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), Juma Pinto na Katibu Msaidizi wa TASWA, George John.
Mwenyekiti wa Chama cha Waadishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), Juma Pinto (kushoto) akizungumza  katika mkutano huo, ambapo aliiomba TBL kuisaidia TASWA kuandaa semina mbalimbali za waandishi wa habari za michezo nchini. Katikati ni Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo. Kulia ni na Katibu Msaidizi wa TASWA, George John.
Akina Dada wanahabari za michezo na burudani wakiwa katika mkutano huo. Kutoka kulia ni Grace Hoka wa magazeti ya Bingwa, Dimba na Mtanzania,  Asha Kigundula wa gazeti la Jambo Leo na Somoe Ng'itu wa Nipashe.

WAKATI tamasha maalum kwa vyombo vya habari ‘Media Day’ kwa mwaka 2012 likipangwa kufanyika Machi 24 kwenye ufukwe wa Msasani, Kampuni ya bia Tanzania (TBL) imetoa shilingi mil.62.5 kwa ajiliya kudhamini tamasha hilo. Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkurugenzi wa Uhusiano wa Jamii na Sheria wa TBL Steven Kilindo alisema kuwa wameamua kudhamini tamasha hilo kutokana na kuthamini mchango wa waandishi wa habari katika biashara za kampuni yao. Alisema kupitia udhamini wao fedha hizo zitatumika katika masuala mbalimbali hivyo watahakikisha linafanya kama ilivyokusudiwa kwani kama ilivyo lengo lake ni kuwakutanisha pamoja watu wa tasnia ya habari, kubadilishana mawazo na pia kupongezana. “TBL itahakikisha bonanza la mwaka huu litafana na litakuwa la aina yake kuanzia katika michezo, burudani, vinywaji na vyakula, hivyo tunawaomba waandishi wajitokeze kwa wingi ili kuweza kubiridika pamoja na kubadilishana mawazi,”Alisema Kilindo. Naye Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo (TASWA) ambayo ndiyo waandaaji wa bonanza hilo Juma Pinto, pamoja na kuishukuru TBL kwa udhamini huo aliiomba kutoishia kudhamini kwenye mabonanza tu bali wafanye hivyo hata katika mafunzo mbalimbali yanayoaandaliwa na chama hicho. “Tunaishukuru TBL kwa kutudhamini katika tamasha letu ambapo mmekuwa mkifanya hivyo kwa miaka kadhaa sasa, lakini tunaomba msiishie katika mabonanza tu kwani tuna semina ambazo tunaziaandaa mara kwa mara na zinahitaji kiasi kido tu cha fedha,”Alisema Pinto. Kwa upande wake Katibu Msaidizi wa Taswa, Geoge John alisema kuwa tamasha hilo litashirikisha waandishi 1500 kutoka vyombo mbalimbali vya habari ambapo kutakuwa na michezo mbalimbali itakayotangazwa baadaye pamoja na burudani ya muziki.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.