TIGO YAWAZAWADIA LAPTOP 16 NA SH. MIL 32 WASHINDI WA PROMOSHENI YA ZAMU YAKO KUSHINDA

Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Tigo, Alice Maro (kushoto), akimkabidhi Mkazi wa Mbagala, Theresia Kagoma zawadi ya kompyuta ndogo baada ya kuwa miongoni mwa washindi wa promosheni ya 'Zamu Yako Kushinda' waliopatiwa zawadi zao Dar es Salaam leo.
Alice Maro (kushoto) akimkabidhi Mkazi wa Mtoni Kijichi, Peter Zephania mfano wa hundi yenye thamani ya sh. mil 4 ambaye ni miongoni mwa wateja 8 waliojishindia katika promosheni ya ZAMU YAKO KUSHINDA

07 Febuari, 2012, Dar es Salaam. Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo imewazawadia washindi nane, kila mmoja shilingi milioni nne, (Tsh. 4,000,000/-) wakiwa ni washindi wa kwanza wa kila siku ambao wamepatikana katika promosheni inayoendelea ya “Zamu yako Kushinda.” Hali kadhalika washindi wengine kumi na sita wamezawadiwa kompyuta aina ya laptop za Samsung. Washindi wamepatikana katika kipindi cha siku 8, na jumla ya fedha zilizotumika kuwalipa washindi mpaka leo ni Shilingi za Kitanzania milioni 264.

“Shindano hili limekuwa na mafanikio makubwa sana,” alisema Alice Maro ambaye ni afisa uhusiano wa kampuni ya Tigo. “Tunapenda kusisitiza kwamba watu waendelee kushiriki kwani bado kuna wiki mbili zaidi kabla ya shindano hili kumalizika,”alisema.

Washindi wa Tsh. 4,000,000/- ni Isack Kaliatano (Tegeta); Benetson Bobelabo (Mbagala); Layakali Thaver (Kariakoo/Livingstone); Faraja Otieno (Arusha); Godfrey Kolawa (Ukonga); Victor Mtundi Zephania (Mtoni Kijichi); Ezekiel Nzige (Mpwapwa) na Suzana Nchala (Sinza Makaburini).

Washindi wa laptop ni Margaret William Msangi (Uwanja wa Ndege); Stanley John Julla (Changanyikeni); Salome Bundala (Yombo Vituka); Peter Mlomo (Magomeni Mapipa); Alli Bakari (Buguruni); Jacqueline Mrema (Kunduchi); Joseph Mambo (Boko); Ramadhani Salum Makusi (Temeke); Maganga Maulidi Kauli (Masaki); Donald Mbwili (Dodoma); Angela Kagaruki (Tabata Segerea); Ibrahim Juma (Ukonga Banana); Dickson Saroty (Gongo la Mboto); Theresia Kagoma (Mbagala); Florentina Soso (Uwanja wa Ndege) na Godfriend Eliamsuli Lyimo (Moshi).
Ili kushiriki mtumiaji wa Tigo anatakiwa kutuma neno “TIGO” kwenda 15571. Gharama kwa kila ujumbe ni Tsh 450. Washiriki wanatakiwa kujikusanyia pointi nyingi ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kujishindia zawadi. Washiriki pia watazawadiwa kutuma ujumbe wa bure kwenda mitandao yote Tanzania.

Watumiaji wa mtandao wa Tigo wenye umri chini ya miaka 18, hawaruhusiwi kushiriki. Promosheni hii ni kwa ajili watumiaji wa Tigo Tanzania.

Kuhusu Tigo:

Tigo ni mtandao wa kwanza wa simu za mkononi Tanzania, ulianzishwa mwaka 1994 ni mtandao wa simu wenye ubunifu wa hali ya juu na wa bei nafuu kupita yote nchini. Tigo ni sehemu ya MillicomInternational Cellular S.A (MIC) na hutoa huduma za simu za mkononi kwa gharama nafuu inapatikana maeneo mengi kiurahisi kwa wateja zaidi ya milioni 30 katika masoko 13 yanayoibuka Afrika na Amerika ya Kusini.

Msingi wa mafanikio ya Tigo ni uzingatiaji wa mikakati mitatu ambayo,ni Gharama nafuu, Uwepo na Upatikanaji .Tunajenga dunia ambapo huduma za simu ni za bei nafuu, zipo na zinapatikana kila mahali na kwa wote. Hii ni kuhakikisha kwamba wateja wetu wanapata huduma bora zaidi kwa bei nafuu kuliko zote katika mikoa yetu 26, Tanzania Bara na Zanzibar.

Kwa taarifa zaidi tembelea: www.tigo.co.tz

Imetolewa na:
Alice Maro • PR-Tigo • Simu 255 715 554501

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

GSM ARIDHIA UJENZI WA UWANJA WA YANGA JANGWANI

WACHEZAJI YANGA WAGOMA KABISA KUFANYA MAZOEZI LEO, LWANDAMINA AIBUKA PEKE YAKE SHAMBA LA BIBI

DKT. MAJULE AMFANYIA MAPOKEZI MAKUBWA BALOZI WA CHINA NCHINI

HERSI KWENDA KUSOMA TENA CHUO KIKUU CHA OXFORD UINGEREZA

UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA MSALATO DODOMA KUANZA KUTUMIKA SEPTEMBA 2026

Wasifu wa Kizza Besigye

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA