Upendo: Nitatoa zawadi Tamasha la Pasaka

Na MWANDISHI WETU

TAMASHA la Pasaka linalotarajiwa kufanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Aprili 8 na 9, mwaka huu na kuhamia uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, limepangwa kusheheni waimbaji wengi wa nyimbo za injili, huku Upendo Kilahiro akitoa zawadi ya albamu yake mpya ya 'Ficho Langu' aliyoirekodi nchini Canada.

Kilahiro ambaye ameahidi kukonga nyoyo za mashabiki atakapopanda jukwaani katika tamasha hilo lililoliandaliwa kwa lengo la kukusanya fedha kwa ajili ya kuwasomesha watoto yatima na kuwasaidia mitaji wajane.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Msama Promotions, ambao ndio waandaaji wa tamasha hilo, Alex Msama, alisema tamasha hilo litasindikizwa na wasanii mbalimbali wa muziki wa injili wa ndani na nje ya nchi.

"Kilahiro tutakuwa naye kwenye tamasha na naamini kwamba mwaka huu tamasha hili litakuwa bora zaidi kutokana na kushirikisha waimbaji wengi wakali," alisema Msama.

Katika mahojiano maalumu Dar es Salaam, Kilahiro alisema amepania kufanya mambo makubwa katika tamasha la mwaka huu na atapanda jukwaani kuimba 'live' na bendi yake ya Upendo Kilahiro.

"Natoa wito kwa mashabiki wangu kutokuwa na wasiwasi, watarajie kupata vitu bora na tofauti zaidi... watapata vitu vinono kwa vile tamasha hili linazidi kuwa bora zaidi.

"Sikukuu ya Pasaka ni upatanisho kutokana na kifo cha Yesu Kristo aliyefia msalabani na kufufuka siku ya tatu... tutaienzi sikukuu hiyo kwa nderemo," alisema Upendo.

Upendo alisema amepania kufanya mambo makubwa kuliko yale aliyofanya katika matamasha yaliyopita ya Sikukuu kama hiyo ambayo ni upatanisho kutokana na kifo cha Yesu Kristo aliyefia msalabani na kufufuka siku ya tatu.

Mwanamuziki huyo anayeabudu katika Kanisa la BCIC lililoko Mbezi Beach, Dar es Salaam (Kwa Askofu Gamanywa), alisema amejiandaa vilivyo kukonga nyoyo za mashabiki wake.

Alitoa wito kwa mashabiki wamiminike kwa wingi uwanjani Aprili 8 na 9 kuona mambo mazuri aliyowaandalia na kuongeza kuwa kwa vile anamtukuza Mungu aliyemtoa kwenye shida na majaribu mengi ya shetani, anaamini atawapa kile wanachotaka kutoka kwake.

Alisema anatarajia kuimba nyimbo mbalimbali zikiwemo zilizotamba za Zindonga (aliyoimba kwa Kizulu), Unajibu Maombi na Ni Salama Rohoni.
Upendo hivi sasa anatamba na albamu yake mpya ya Ficho Langu aliyoirekodi nchini Canada.

Wasanii wengine wa nyimbo za Injili atakaopamba tamasha hilo wanatarajiwa kutangazwa wakati wowote wakiwamo waimbaji kutoka nchi za Kenya, Uganda, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), Afrika Kusini na Zambia.

ciao

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.