Upendo Nkone kupamba tamasha la Pasaka

Na Mwandishi Wetu

MWANAMUZIKI wa nyimbo za Injili nchini, Upendo Nkone anatarajiwa kuwa miongoni mwa waimbaji watakaopamba tamasha la Pasaka linalotarajiwa kufanyika Aprili 8 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mratibu wa tamasha hilo, Alex Msama wa Kampuni ya Msama Promotions, alisema Dar es Salaam jana kuwa Nkone amekuwa mwimbaji wa pili kuthibitisha kushiriki tamasha hilo baada ya Upendo Kilahiro.

Msama ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, alisema anaamini tamasha la mwaka huu litakuwa bora zaidi kwa vile litashirikisha waimbaji wengi wakali.

Tamasha hilo la aina yake, baada ya kufanyika Dar es Salaam, pia litarindima kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Aprili 9 mwaka huu.

Tamasha la Pasaka mwaka huu malengo yake makubwa ni kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwasomesha watoto yatima na kuwasaidia mitaji wanawake wajane.

Msama alisema tamasha hilo pia litashirikisha waimbaji wa nyimbo za Injili kutoka nchi kadhaa za Afrika ikiwa ni pamoja na Kenya, Uganda, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Afrika Kusini na Zambia.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Nkone alisema anaendelea vyema na maandalizi kwa ajili ya tamasha hilo, na akatoa mwito kwa mashabiki wake wasiwe na wasiwasi, watarajie kupata mambo mazuri zaidi.

Aliwaomba mashabiki wamiminike kwa wingi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Aprili 8 na Jamhuri Aprili 9, kuona mambo mazuri aliyowaandalia.

Ciao...

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.