WANAHABARI WASHINDANA KUONJA BIA TBL MBEYA

Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Edith Mushi akimkabidhi katoni ya bia mwandishi wa habari wa gazeti la Dira ya Mtanzania, Steve Jonas ambaye alikuwa ni mshindi wa pili kati ya washindi watatu waliofanikiwa kubaini ladha halisi ya bia zinazotengenezwa na kampuni hiyo Jijini Mbeya mwishoni mwa wiki.

Mshindi wa kwanza wa uonjaji ladha halisi za Bia zinazotengenezwa na Kampuni ya TBL Mbeya ambaye ni mwandishi wa habari wa Chanel Ten Saada Matiku akipokea katoni za Bia kutoka kwa Meneja wa kiwanda cha Bia mkoani Mbeya Calvin Martin, Matiku alizawadiwa katoni
tatu za Bia.
Wanahabari wakishindana kuonja bia
Mwandishi wa habari wa gazeti la Tanzania Daima Christopher Nyenyembe(kushoto) na mwandishi wa habari wa gazeti la Raha Tele George Chanda (katikati) wakionja Bia zinazotengenezwa na kampuni ya Bia Tanzania TBL katika shindano la kumtafuta muonjaji mahiri wa Bia za kampuni anayeangalia kulia ni Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Edith Mushi.
Mwandishi wa habari wa Gazeti la Habari Leo Joachim Nyambo akipokea zawadi ya katoni ya Bia aina ya Ndovu kutoka kwa Meneja Uhusiano na Mawasiliano Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Edith Mushi baada ya kuibuka mshindi wa kubaini ladha halisi ya aina ya vileo vinavyotengenezwa na kampuni ya Bia ya TBL.Mashindano hayo yaliyohusisha wannahabari wa mkoa huo yalifanyika mwishoni mwa wiki.
Wanahabari wakiangalia moja ya mitambo ya kupikia bia
Meneja wa Kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Mbeya, Calvin Martine akitoa maelezo kwa waandishi wa habari wa Mkoa wa Mbeya, kuhusu uzalishaji wa bia walipotembelea kiwanda hicho, mwishoni mwa wiki.

Meneja wa Kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Mbeya, Calvin

Martine akitoa maelezo kwa waandishi wa habari wa Mkoa wa Mbeya, kuhusu

uzalishaji wa bia walipotembelea kiwanda hicho, mwishoni mwa wiki.

Baadhi ya Waandishi wa habari wa Jijini Mbeya wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa kampuni ya uzalishaji vileo ya TBL wakati wa kubaini ladha halisi ya vileo vinavyozalishwa na kampuni hiyo.
Baadhi ya waandishi wa habari wa jijini Mbeya wakitembelea kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kilichopo Iyunga jijini humo mwishoni mwa wiki.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI