Watafiti wa kimataifa watua Samunge

WATAFITI wa kimataifa wa masuala ya tiba na wanahabari kutoka Japan wamefika Samunge kuendelea kutafiti dawa inayotolewana Mchungaji Ambilikile Masapila.

Mmoja wa wasaidizi wa Mchungaji Masapila, Paulo Dudui, alisema Wajapani hao wamefika hivi karibuni na watafiti wengine tokanchi za ulay ikiwepo Ujeremani na Uingereza .

“Wanakuja watafiti wanachukua dawa wanasema wamepata taarifa za dawa hizo wakiwa nchi kwao,” alisema Dudui.
Akizungumzia tiba hiyo, Dudui alisema bado inatolewa ingawa ni watu wachache wanaofika.
“Watu wanakuja na babu bado anasema kuna miujiza mingine itakuja na anaendelea na ujenzi wa kituo kipya cha tiba,” alisema Dudui.

Kampuni ya Simu ya Vodacom haitafunga huduma zake Kijiji cha Samunge , wilayani Ngorongoro, ambako maelfu ya watu walikuwa wakifika kupata kikombe cha tiba kwa Mchungaji Masapila licha ya sasa watu kupungua na wanaofika wengi ni watafiti.

Kampuni kadhaa ya simu zilifikisha huduma zake Samunge kuanzia Mei mwaka jana kutokana na kufurika kwa watu kupata kikombe cha tiba, lakini sasa baadhi ya kampuni zimesitisha huduma eneo hilo.
Mkurugenzi wa Vodacom Kanda ya Kaskazini, Nguvu Kamando, alisema wakazi wa Samunge wataendelea kupata huduma zote za kampuni hiyo.

“Ni kweli kuwa hivi sasa kuna wateja wachache Samunge na ni gharama kuendesha mtambo kule, lakini Vodacom hatutafunga mawasiliano kwani kuna wateja wetu wengi eneo hilo,” alisema Kamando.

Alisema wateja hao na wengine wa Mkoa wa Arusha na maeneo mengine, wamekuwa wakinufaika na huduma za kampuni hiyo, ikiwapo ya kutuma na kupokea fedha kupitia simu zao.

Awali, Meneja wa Vodacom Arusha, Jerome Munishi, alisema kampuni hiyo mkoani hapa ina mawakala 600 ambao wamekuwa wakitoa huduma mbalimbali.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI