Waume walalamikia kipigo Kenya

Februari tarehe kumi na nne ni siku ya wapendanao au Valentine, lakini siku hii ikiadhimishwa kote duniani kwa raha, baadhi ya waume nchini kenya hawaifurahi kwani wanapigwa na kunyanyaswa na wake zao.

Kulingana na mwenyekiti wa chama cha kutetea haki za wanaume nchini humo Nderitu Njogu, idadi ya wanaume wanaopigwa na wake zao imeongezeka mno.

Bw Nderitu anasema utafiti wa chama chake umeonyesha kuwa harakati za kumpa uwezo mwanamke zimeathiri maadili na kuwasabibisha kuwadharau wanaume.

Mwanaharakati huyo anadai kuwa tatizo hilo limechochewa zaidi na hali ya kuwa wanawake wengi sasa wana kipato kikubwa kuliko waume zao.

Mwishoni mwa wiki Polisi walimtia mbaroni mwanamke mmoja mjini Nyeri huko mkoa wa kati, baada ya kumshambulia mumewe na kumjeruhi vibaya kwa panga.

Mwanamume huyo bado anapokea matibabu hospitalini baada ya kukatwa katwa usoni. uchunguzi kuhusu tukio hilo bado unaendelea.

Bw Nderitu anadai kuwa zaidi ya wanaume 460,000 walinyanyaswa na wake zao mwaka jana. Anasema utafiti wa shirika lake unaonyesha kesi nyingi za waume kuteswa na wake zao zinaripotiwa katika mkoa wa kati.

"Siku hii ya Valentine na washauri wanaume wasikubali kudhalalishwa na wake zao, kwa kufanya matumizi makubwa kuliko na wanayoweza kumudu" alisema Bw Nderitu.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*